Mkataba wa Januari huenda unaandaliwa na Liverpool kumsajili kiungo wa kati wa England Jude Bellingham kutoka Borussia Dortmund, 19. (Football Insider)
Mshambulizi wa zamani wa Liverpool Emile Heskey anasema The Reds “wanamwinda” Bellingham. (Mirror)
Liverpool na Juventus wanafuatilia mazungumzo ya kandarasi yanayoendelea kati ya kiungo wa kati wa Uingereza Mason Mount, 23, na Chelsea. (Guradian)
Chelsea inamwona Mount kama nahodha wa siku zijazo wa klabu lakini mkataba wake wa sasa unaifanya Blues Academy kuwa miongoni mwa wachezaji wanaolipwa mshahara wa chini zaidi kwenye kikosi hicho. (Mail)
Kocha wa zamani wa Tottenham, Southampton na Paris St-Germain Mauricio Pochettino anasema “atakuwa wazi kwa kila kitu” alipoulizwa kama angependa kuwa meneja wa Uingereza. (Athletic Sunscription Required)
Fulham, Bayer Leverkusen na Villarreal wana nia ya kumsajili beki wa kulia wa Ureno Cedric Soares, 31, kutoka Arsenal mwezi Januari. (ESPN)
Aston Villa ilikataa nafasi ya kumsajili kiungo wa kati wa Ureno Joao Palhinha kabla ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kujiunga na Fulham. (Football Insider)
Mshambulizi wa zamani wa Barcelona na Liverpool Luis Suarez, 35, amekataa ofa ya kujiunga na klabu ya Gremio ya Brazil mara tu mkataba wake na Nacional ya nchini kwao Uruguay utakapokamilika. (Fabrizio Romano)
Source; BBC SWAHILI