Manchester United wanaweza kufikiria kuvunja mkataba wa fowadi wa Ureno Cristiano Ronaldo kufuatia mahojiano yake na Piers Morgan lakini watasubiri hadi watakaposikia mahojiano kamili kabla ya kufanya uamuzi kuhusu mustakabali wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37. (Telegraph – subscription)
Ronaldo anaweza kwenda Chelsea baada ya fowadi huyo kuhusishwa na kuhamia Stamford Bridge majira ya joto lakini iliripotiwa kuzuiwa na meneja wa wakati huo Thomas Tuchel. (CBS via Express)
Manchester United wameungana na Arsenal kumsaka winga wa Shakhtar Donetsk na Ukraine Mykhaylo Mudryk, huku mkufunzi wa United Erik ten Hag akisemekana kumtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 tangu alipokuwa meneja wa Ajax. (Sun)
Manchester City wanapanga mazungumzo na wakala wa kiungo wa kati wa Ureno Bernardo Silva wakati wa Kombe la Dunia ili kuamua mpango wa maisha yake ya baadaye. Mabingwa hao wa Premier League wanafahamu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 anataka kujiunga na Barcelona na hatamzuia iwapo ofa sahihi itatolewa. (Mundo Deportivo – AS Spain)
Beki wa kulia wa Leeds United Muingereza Cody Drameh, 20, anavutiwa na Newcastle United, pamoja na Lille, Borussia Dortmund na Bayer Leverkusen. (Fabrizio Romano)
Thomas Tuchel lazima aondoke Uingereza mwezi Disemba, kutokana na sheria za baada ya Brexit, baada ya kutimuliwa Chelsea, lakini makocha wake wawili, Zsolt Low na Benjamin Webber, ambao wamepewa likizo ya bustani, wanaweza kubaki kwa sababu bado wako chini ya mkataba wa kiufundi. (Telegraph – Subscription required)