Manchester City wanahofia Ilkay Gundogan ataondoka katika klabu hiyo kwa uhamisho wa bila malipo msimu ujao. Kiungo huyo wa kati wa Ujerumani, 32, bado hajakubali mkataba mpya, na mkataba wake wa sasa unamalizika Juni. (Football Insider)
Manchester United wanataka kupata hatima ya Marcus Rashford Old Trafford kabla ya mwisho wa mwaka ili kumzuia kunyakuliwa. Mshambulizi huyo wa kimataifa wa Uingereza, 25, atakuwa huru kufanya mazungumzo na vilabu vya kigeni mwezi Januari isipokuwa iwapo atatia saini mkataba mpya au kipengele cha chaguo la mwaka mmoja katika kandarasi yake. (Daily Mail)
Manchester United wana nia ya kumsajili beki wa kulia wa Uingereza Max Aarons, 22, kutoka Norwich ili kumpa changamoto mchezaji wa kimataifa wa Ureno Diogo Dalot, 23, huku Mholanzi wa Bayer Leverkusen Jeremie Frimpong, 21, akiwa chaguo lingine. (Sun)
Arsenal wameripotiwa kutuma maskauti kumtazama kiungo wa kati wa Palmeiras na Brazil Danilo wiki iliyopita, huku The Gunners wakiwa na nia ya kumleta mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 mwezi Januari. (Sun)