Mshambulizi wa Brentford Ivan Toney, 26, yuko tayari kwenda Kombe la Dunia akiwa na England licha ya uchunguzi na FA kuhusu kushiriki kamari. (Sun)
Winga wa Crystal Palace na Ivory Coast Wilfried Zaha, 29, anakataa kubashiri juu ya mustakabali wake licha ya kandarasi yake kumalizika msimu wa joto. (Sky Sports)
West Ham wanapanga kumnunua mshambuliaji wa Blackburn Rovers na Chile Ben Brereton Diaz, 23 katika dirisha lijalo la mwezi Januari (Football Insider)
Leeds inaongoza katika kinyang’anyiro cha kumsajili kiungo wa kati wa Birmingham, 18, Muingereza George Hall. (Sun)
Southampton imeamua kumfukuza kazi meneja Ralph Hasenhuttl baada ya kichapo cha mabao 4-1 kutoka kwa Newcastle siku ya Jumapili na kuiacha klabu hiyo katika hatari ya kushuka daraja. (Athletic)
Newcastle United na Aston Villa zinataka kumrejesha ligi kuu ya England mshambuliaji wa Real Madrid na Ubelgiji Eden Hazard, 31. (El Nacional)
Tottenham wanafikiria kumnunua winga wa Everton Muingereza Anthony Gordon, 21, katika dirisha la uhamisho la Januari. (Sun
Arsenal bado inataka kumsajili winga wa Shakhtar Donetsk na Ukraine Mykhaylo Mudryk, 21. (CaughtOffside)