Mshambulizi wa zamani wa Liverpool na Barcelona Luis Suarez, 35, alikataa ofa kutoka kwa Gremio kwa sababu raia huyo wa Uruguay atajiunga na klabu ya MLS, meneja wa klabu hiyo ya Brazil amesema. (Bild)
Wakala wa kiungo wa Dynamo Moscow na Urusi Arsen Zakharyan ametaja nia ya Chelsea kumnunua mchezaji huyo wa miaka 19 “hadithi tata”. (Champion)
AC Milan wanafikiria kumchukua kwa mkopo mwezi Januari winga wa Chelsea Hakim Ziyech, 29, na kumnunua mshambuliaji wa The Blues mwenye umri wa miaka 21 raia wa Albania Armando Broja. (Corriere Dello Sport)
Milan pia wanavutiwa na kiungo wa kati wa Chelsea Muingereza Ruben Loftus-Cheek, 26, baada ya kuonyesha kiwango kizuri dhidi yao kwenye Ligi ya Mabingwa huko Stamford Bridge. (Calciomercato)