Borussia Dortmund huenda ikahitaji dau la rekodi ya £130m kutoka kwa ligi ya Uingereza ili kumuuza kind awa Uingereza Jude Bellingham, 19, anayevutia Manchester United, Chelsea na Liverpool..(Sun)
Kipa wa Uhispania David de Gea, 31, yuko tayari kupunguza mshahara wake wa pauni 375,000 kwa wiki katika klabu ya Manchester United ili kuongeza muda wake wa kukaa Old Trafford. (Athletic, via Sun)
Chelsea wanapewa nafasi kubwa ya kumsajili kiungo wa kati wa Juventus na Ufaransa Adrien Rabiot, 27, katika dirisha la uhamisho la Januari. (Fichajes – in Spanish)
Everton na Newcastle United wanamfuatilia mshambuliaji wa Chelsea na Albania Armando Broja, 21CBS Sports)
Unai Emery ametia saini mkataba wa angalau miaka minne na nusu, mkataba mrefu zaidi wa ukufunzi katika historia ya Aston Villa, huku akijiandaa kuanza kazi yake rasmi wiki hii. (Telegraph – subscription required)
Chelsea wameanzisha dau la pauni milioni 30 kumnunua mshambuliaji wa Brighton na Ubelgiji Leandro Trossard, 27. (FourFourTwo)
Barcelona wanamtazama mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta, 40, kama mbadala wa meneja wao Mhispania Xavi Hernandez, 42.. (Sport)
Matumaini ya Arsenal na Chelsea kumsajili fowadi wa Ivory Coast Wilfried Zaha yameongezeka, kwani mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 bado hajakubali kuongezewa mkataba katika klabu ya Crystal Palace licha ya kuombwa kuongezwa mkataba mpya kwa maneno. (Mail)
SOURCE; BBC SWAHILI