Kampuni ya Mawasiliano, Tigo Tanzania imeshiriki katika maonesho ya wiki ya huduma za kifedha yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango yanayoendelea jijini Mwanza.
Tigo Pesa ikiwa ni huduma kamili ya kifedha, mkakati wa kampuni hio ni kusogeza huduma zake karibu na wateja wake sambamba na kutoa elimu na kuwaongezea watanzania uelewa juu ya masuala ya kifedha kwa njia ya simu.
Imesisitiza kuweza kufurahia huduma za kifedha na za kidigitali kama vile Kibubu, ,Bustisha), Nivushe pamoja na Lipa kwa simu zinazopatikana nchi nzima.
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT