Kiungo wa Manchester City na Ureno, Bernardo Silva amesema wanakwenda kucheza kombe la Dunia 2022 kwa ajili ya Cristiano Ronaldo.
–
Silva anasema atapambana kwa ajili ya Ronaldo sio kwa ajili yake binafsi.
–
“Tunakwenda kucheza kombe hili la Dunia kwa ajili ya Cristiano Ronaldo. Nitapambana kwa ajili ya Ronaldo sio kwa ajili yangu binafsi.” Amesema Silva.
–
Ronaldo (37) atakuwa anashiriki kombe la Dunia kwa mara ya 5 na huenda toleo la 2022 la kombe la Dunia likawa la mwisho kwake kushiriki hivyo itapendeza ikiwa atastaafu akiwa ameshinda taji hilo.
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT