Idadi ya mbegu za kiume duniani kote inapungua kwa kasi ya kiwango cha asilimia 50 katika kipindi cha miaka 40 iliyopita, utafiti mpya umebaini.
–
Utafiti huo umeonyesha kwa mwaka 2018 mwanaume alitoa mbegu milioni 33 hadi milioni 46 katika kila mililita ya manii, kiwango ambacho pia kimetajwa kupungua kwa asilimia 50 kwa sasa ikilinganishwa na utafiti wa mwaka 1973, ambapo alizalisha mbegu milioni 101.1 kwa mililita.
–
Wakati ripoti hiyo ikichapishwa katika jarida la Human Reproduction Update Novemba 15, hapa nchini kumekuwa na ongezeko la wanaume wanaopata changamoto hiyo kutokana na mtindo wa maisha na ongezeko la joto kwa mujibu wa daktari bingwa wa fiziolojia ya homoni na mazoezi kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Fredrick Mashili.
–
Mkuu wa Kitengo cha magonjwa na kinamama na uzazi Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk Nathanael Mtinangi alisema changamoto hiyo nchini inaonekana pia, kwa sababu asilimia 50 ya wagumba wanaogundulika ni wanaume.
–
Source : Mwananchi