Kampuni ya Mawasiliano nchini, Vodacom Tanzania imeishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuona mchango wake katika uchumi wa nchi na kuipa nafasi ya kushiriki mkutano wa Diplomasia ya Uchumi na kuonyesha jinsi huduma zake za kifedha hususani kutuma na kupokea pesa Afrika na duniani kote zinavyoweza kuwapa wafanyabiashara masoko na uwezo wa kutanua biashara zao.