ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Saturday, April 1, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

Washindi 75 wa NMB MastaBata KoteKote wamechomoka na Laki moja kila mmoja na Pikipiki

I am Krantz by I am Krantz
Nov 14, 2022
in HABARI
0
Washindi 75 wa NMB MastaBata KoteKote wamechomoka na Laki moja kila mmoja na Pikipiki
0
SHARES
38
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard, akibonyeza kitufe cha kompyuta kuchezesha droo ya kwanza ya Kampeni ya NMB MastaBata ‘Kote Kote’ inayohamasisha matumizi ya kadi badala ya pesa taslimu, iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa NMB Tawi la Mlimani City, Deogratius Kawonga na Kulia ni Meneja Mwandamizi Idara ya Kadi na Biashara wa NMB, Manfredy Kayala.

Zawadi zenye thamani ya Sh. Mil. 10.5 za droo ya kwanza ya Kampeni ya NMB MastaBata ‘Kote Kote’ zimepata wenyewe mwishoni mwa wiki, ambapo washindi 76 walipatikana, 75 kati yao wakijishindia fedha kiasi cha Sh. Mil. 7.5, huku Asumwisye Stallone akiibuka na zawadi ya bodaboda yenye thamani ya Sh. Mil. 3.

Kampeni hiyo, ambayo inaendeshwa na Benki ya NMB kwa ushirikiano na Mastercard International, ikilenga kuhamasisha matumizi ya NMB Mastercard kufanya malipo, Lipa Mkononi kwa kuskani QR na kufanya malipo mtandaoni huku zawadi mbalimbali zenye thamani ya zaidi ya Sh. Mil. 350 zitatolewa katika miezi mitatu ya kinyang’anyiro hicho.

RelatedPosts

YANGA TUNAHITAJI KUIFUNGA MAZEMBE TUONGOZE KUNDI

YANGA TUNAHITAJI KUIFUNGA MAZEMBE TUONGOZE KUNDI

Apr 1, 2023

GARI LA KIFAHARI ZAIDI NA LENYE THAMANI KUBWA

Apr 1, 2023

ONYANGO AOMBEWA MSAMAHA KWA ALICHOFANYA

Apr 1, 2023
Load More

Akizungumza kabla ya droo hiyo, Meneja Mwandamizi wa Biashara ya Kadi wa NMB, Manfredy Kayala, alisema malengo makuu ya kampeni hiyo iliyoanzishwa mwaka 2018, ni kuihamasisha jamii katika kuachana na matumizi ya pesa taslimu ‘cashless’, lakini pia ikilenga kurejesha sehemu ya faida yao kwa wateja wao.

Kayala alifafanua kuwa, ukiondoa bodaboda moja na pesa taslimu kwa washindi 75 wa kila wiki, NMB MastaBata Kote Kote itatoa zawadi kwa washindi 49 wa droo za mwisho wa mwezi, sambamba na bodaboda mbili, na droo ya fainali itazawadia safari za Dubai kwa washindi na wenza wao kwa siku nne.

ADVERTISEMENT

Mbele ya Ofisa wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard, alisema NMB MastaBata Kote Kote ni muendelezo wa benki yake katika kuwafanya wateja na Watanzania kugeukia utamaduni chanya wa matumizi yasiyohusisha pesa taslimu.

Alifafanua kuwa, MastaBata Kote Kote inagusa wateja wote wa ndani na nje ya nchi wanaotumia kadi za Mastercard au Lipa Mkononi kaa kuscan QR na kutoa wito kwa Watanzania kuhakikisha wanatumia kadi zao katika kufanya malipo na miamala mbalimbali ili kujiweka kwenye nafasi ya kushinda.
Kampeni hii ya NMB MastaBata KoteKote itaendelea kwa takribani miezi mitatu. Kutakuwa na washindi wa kila wiki, kila mwezi na na wale wa Grand Finale. Wateja wanapaswa kufanya malipo kwa kadi Ya NMB Mastercard au Lipa Mkononi (mastercard QR) ili kujiwekea nafasi ya kushinda.

Mwisho

ADVERTISEMENT

Related

I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

YANGA TUNAHITAJI KUIFUNGA MAZEMBE TUONGOZE KUNDI
HABARI

YANGA TUNAHITAJI KUIFUNGA MAZEMBE TUONGOZE KUNDI

by Shabani Rapwi
Apr 1, 2023
GARI LA KIFAHARI ZAIDI NA LENYE THAMANI KUBWA
HABARI

GARI LA KIFAHARI ZAIDI NA LENYE THAMANI KUBWA

by Shabani Rapwi
Apr 1, 2023
ONYANGO AOMBEWA MSAMAHA KWA ALICHOFANYA
HABARI

ONYANGO AOMBEWA MSAMAHA KWA ALICHOFANYA

by Shabani Rapwi
Apr 1, 2023
KOCHA NABI NA WACHEZAJI HAWA KUKOSA MCHEZO DHIDI YA MAZEMBE, SABABU YATAJWA
HABARI

KOCHA NABI NA WACHEZAJI HAWA KUKOSA MCHEZO DHIDI YA MAZEMBE, SABABU YATAJWA

by Shabani Rapwi
Apr 1, 2023
TANI 20.6 ZA BANGI ZIMEKAMATWA 2022
HABARI

TANI 20.6 ZA BANGI ZIMEKAMATWA 2022

by Shabani Rapwi
Apr 1, 2023
SAFU YA ULINZI IMEWAANGUSHA SIMBA
HABARI

SAFU YA ULINZI IMEWAANGUSHA SIMBA

by Shabani Rapwi
Apr 1, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
November 2022
M T W T F S S
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
282930  
« Oct   Dec »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In