Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inategemea pato la nchi kwa asilimia 29.2% katika sekta ya Utalii huku akieleza kuwa Serikali imeweka hatua za makusudi katika mazingira wezeshi kwa kujumuisha sera,mifumo ya kitaasisi na kisheria ili sekta hiyo ikue kwa njia endelevu.
ADVERTISEMENT
Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo katika Kongamano la Kimataifa la 22 la WORLD
Travel &Tourism Council Global Summit lililofanyika jijini Riyadh,Saudi Arabia katika Hoteli ya Ritz-Carlton ambapo amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan.

Aidha, alisema ukuaji wa sekta ya Utalii inatarajiwa kuwavutia wageni wenye uwezo mkubwa ambao watatumia fedha zaidi ili kulinda rasilimali za bahari pamoja na uchafuzi wa Mazingira.
Akifungua Kongamano hilo Waziri wa Utalii wa Saudia Arabia Mhe.Ahmed Al Khateeb amesema anatarajia majadiliano ya Kongamano hilo yatoe njia sahihi za kutatua changamoto za Utalii,Usafirishaji na Mazingira kwa ujumla.
Pia,Kongamano hilo limehudhuriwa na Viongozi kutoka Mataifa mbalimbali Duniani ambapo walipata fursa ya Kuchangia .
Kongamano hilo la 22 la WORLD
Travel &Tourism Council Global Summit limeongozwa na Mwandishi nguli nchini Marekani wa CBS ,Peter Greenberg ambaye alikuwa mtayarishaji wa filamu ya Royal Tour Tanzania

28 November 2022
Ritz-Carlton, Riyadh Saudi Arabia

President of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council Dr. Hussein Ali Mwinyi has said that the Revolutionary Government of Zanzibar depends on 29.2% of the country’s revenue in the tourism sector while explaining that the government has put deliberate steps in Mazi. Enhance policies, institutional and legal systems in this sector let that grow in a sustainable way.\nPresident Dr. Mwinyi has said this at the 22nd International Conference of the WORLDTravel & Tourism Council Global Summit that took place in Riyadh, Saudi Arabia at Ritz-Carlton Hotel where he has represented the President of the Republic of Tanzania Honorable. e. Samia Suluhu Hassan.
In addition, he said the growth of tourism sector is expected to attract potential visitors who will use more funds to protect marine resources as well as environmental pollution.Opening the conference, the Minister of Tourism of Saudi Arabia Honorable Ahmed Al Khateeb has said that he expects the conference discussions to provide the right ways to solve the challenges of tourism, transportation and environment in general.Also, the conference has been attended by leaders from different nations of the world where they got the opportunity to contribute.The 22nd WorldTravel & Tourism Council Global Summit has been led by the best writer in America of CBS, Peter Greenberg who was a producer of the film Royal Tour Tanzania.
28 November 2022
Ritz-Carlton, Riyadh Saudi Arabia
ADVERTISEMENT