Timu ya Taifa ya Argentina imefanikiwa kutinga hatua ya michuno ya Fainali za Kombe la Dunia chini ya FIFA 2022 baada ya kuilaza timu ya Taifa ya Croatia kwa jumla ya Goli 3-0.
Magoli yalioofungwa na nyota Leonel Messi 34′(P) pamoja na Juli’an ‘Alvarez 39’, 69, yameifanya Argrntina kutinga mnamo hatua hio kibabe zaidi.
Ikumbukwe kuwa hii imekuwa ni moja ya Furaha kubwa kwa kikosi cha timu ya Taifa ya Argentina kushinda dhidi ya Croatia kwani katika rekodi za michuano ya fainali za kombe la Dunia Argentina iliwahi kutolewa na Croatia kwa ushindi wa bao 3 ilopelekea Argentina kushindwa endele na michuano ijayo.
Kwa sasa Argentina inasubiri timu mojawapo itakayoshinda katika mchezo wa nusu fainali kati ya Timu ya Ufaransa na Morocco ili kuweza kuchuana nayo vilivyo.