Benki ya Equity Tanzania imetangaza uteuzi wa Isabela Maganga kama Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hio. Kabla ya kuteuliwa, aliwahi kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Equity Tanzania na awali akiwa Mkuu wa Kitengo cha Biashara.
Akizungumzia uteuzi huo, mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Equity Tanzania Eng. Raymond Mbilinyi alibainisha kuwa bodi ina imani kwamba ujuzi na uzoefu wake wa nguvu utakuwa muhimu tunapoendelea na mipango yetu ya kukuza Benki na kuhudumia watu zaidi kulingana na madhumuni yetu ya kubadilisha maisha, kujitoa kwa weledi na kupanua fursa za uzalishaji mali.