ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Monday, February 6, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

Benki ya NBC Yazindua Kampeni ya Funga Mwaka Kibabe

Dar es Salaam, Tanzania

ALFRED MTEWELE by ALFRED MTEWELE
Dec 5, 2022
in BIASHARA
0
Benki ya NBC yazindua kampeni ya Funga Mwaka Kibabe na NBC
0
SHARES
49
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kidijitali wa Benki ya NBC, Ulrik Tobias (katikati) ,Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya kibenki ya kidijitali inayoitwa “Funga Mwaka Kibabe na NBC Bank.” Kampeni hii inalenga kukuza matumizi ya chaneli za kidijitali mtandaoni kwa wateja wa Benki ya NBC wakati wa msimu wa sikukuu.Pembeni kulia yake ni Kaimu Mkuu wa kitengo cha masoko David Raymond na maafisa wengine wa Benki hiyo wakishuhudia uzinduzi huo.Uzinduzi huo ulifanyika mwishoni wa wiki iliyopita Jijini Dar es salaam.
  • Benki ya NBC yazindua kampeni ya kibenki ya kidijitali kuzawadia zaidi ya wateja 400
  • Kampeni itaendeshwa nchi nzima
  • Kupitia NBC Kiganjani na huduma za kibenki kupitia simu wateja wanaweza kufanya malipo ya bili

Dar- es – Salaam – Disemba 2022. Katika juhudi za ku

kuza miamala ya papo kwa papo, salama na malipo ya bila kutumia  pesa taslimu nchini, Benki ya NBC imezindua kampeni yake mpya ya kibenki ya kidijitali inayoitwa “Funga Mwaka Kibabe na NBC Bank.” Kampeni hii inalenga kukuza matumizi ya chaneli za kidijitali mtandaoni kwa wateja wa Benki ya NBC wakati wa msimu wa sikukuu. Mapinduzi mapya ya malipo yanayofanyika

RelatedPosts

Benki ya NBC Yahitimisha Kampeni ya ‘Vuna Zaidi na NBC Shambani’

Benki ya NBC Yahitimisha Kampeni ya ‘Vuna Zaidi na NBC Shambani’

Jan 27, 2023

Benki ya NBC imetoa mafunzo kwa mashirika zaidi ya 100 ya bima ili kuimarisha upatikanaji wa huduma hiyo nchi nzima

Nov 23, 2022

Serikali Yatambua Mchango wa Benki ya NBC Katika Sekta ya Viwanda Nchini

Nov 21, 2022
Load More

kupitia viza ( Visa) yatawahakikishia usalama wateja na urahisi zaidi wa kufanya malipo. Katika jitihada za kukuza miamala salama na ya papo kwa papo isiyotumia  nguvu nyingi, na malipo ya bila kutumia pesa taslim nchini!

Kupitia kampeni hii mpya, wateja wa Benki ya NBC wanaofanya miamala kupitia njia mbadala za kidijitali za NBC Kiganjani,huduma ya benki kupitia mtandao na kupitia kadi ya NBC Debit watapata fursa ya kujishindia zawadi za pesa taslimu, simu za mkononi, luninga na mengine mengi.

 

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ka

mpeni hiyo, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kidijitali wa Benki ya NBC, Ulrik Tobias, alisema kampeni hiyo mpya inalenga kuhakikisha wateja wanaweza kupata pesa zao kwa usalama na kufanya miamala kwa urahisi, kuongeza urahisi zaidi wa huduma na kuboresha uzoefu kwa wateja.

 

“Tunataka kuwapa wateja wetu muda wa kutosha kwa ajili ya familia na wapendwa wetu katika msimu huu wa sikukuu kwa kuwahakikishia kwamba wanaweza kufanya miamala yote ya benki wakiwa katika hali ya starehe wakiwa majumbani mwao. Tunaelewa kuwa wengi watakuwa likizoni na pengine kujiingiza katika matembezi mengi ya matumizi katika wakati huu. Benki ya NBC imehakikisha kuwa unaweza kufanya miamala kwa urahisi na kwa ufanisi ukiwa nyumbani huku ukipata nafasi ya kujishindia zawadi”. Alisema Ulrik.

 

Ulrik pia aliongeza kuwa kampeni hiyo inalenga kuwazawadia watumiaji. Kadiri unavyofanya miamala mingi, ndivyo unavyojishindia na kupokea zawadi za kampeni kama vile simu za mkononi, luninga, punguzo la asilimia 40 kwa ununuzi mbalimbali, zawadi za pesa taslimu na vocha za kufanyia manunuzi.

“Wateja wote wanaotumia kadi zetu za benki za visa, ATM, App ya NBC ya simu, na huduma za NBC Kiganjani watakuwa na nafasi sawa za kushinda zawadi hizi. Wanachotakiwa kufanya ni kufanya miamala. Kutakuwa na droo za kila wiki, droo za kila mwezi, na zawadi za papo hapo zitashindaniwa. Tunalenga kuwazawadia zaidi ya wateja 400 waaminifu. Tutahakikisha kuwa kuna miamala isiyo na matatizo katika msimu huu wa sikukuu ili wateja wetu waweze kufurahia na kupata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali kwa kutumia chaneli za kibenki za kidijitali.” Alisema Ulrik.

 

Kampeni itaanza tarehe 2 Desemba 2022 hadi Januari 26, 2023. Benki imeshirikiana na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania ili kuhakikisha kwamba ushindi wote ni wa haki na wa wazi. Washindi watatangazwa na kutunukiwa hadharani.

ADVERTISEMENT

 

Funga mwaka Kibabe ni mpango wa NBC unaolenga kuboresha uzoefu wa kibenki wa kidijitali kwa wateja kupitia chaneli mbalimbali. Kampeni hii inajikita katika kutoa suluhisho za kufanya miamala kidigitali ambapo pia  wateja wanapata nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali haswa msimu huu wa sikukuu.

ADVERTISEMENT

 

Zawadi zitapatikana kupitia droo za bahati nasibu za kila wiki na kila mwezi ambapo wateja lazima wawe wamefanya miamala zaidi ya mara 20 hadi 70 ili kuboresha nafasi zao za kushinda.

Related

Tags: NBC Bank
ADVERTISEMENT
ALFRED MTEWELE

ALFRED MTEWELE

Related Posts

NMB yafadhili ziara ya mafunzo Machinga, Bodaboda Dar nchini Rwanda
BIASHARA

NMB yafadhili ziara ya mafunzo Machinga, Bodaboda Dar nchini Rwanda

by I am Krantz
Feb 3, 2023
Benki ya NMB Yakabidhi Tiketi kwa Viongozi 12 Kwenda Rwanda na Kurudi
BIASHARA

Benki ya NMB Yakabidhi Tiketi kwa Viongozi 12 Kwenda Rwanda na Kurudi

by ALFRED MTEWELE
Feb 3, 2023
TANZANIA COMMERCIAL BANK YATOA MSAADA WA MIFUKO 100 YA CEMENT UJENZI WA KITUO CHA POLISI KIBURUGWA
BIASHARA

TANZANIA COMMERCIAL BANK YATOA MSAADA WA MIFUKO 100 YA CEMENT UJENZI WA KITUO CHA POLISI KIBURUGWA

by Ally Hamis Zingizi
Jan 27, 2023
TANZANIA COMMERCIAL BANK YAIPIGA JEKI SEKTA YA ELIMU YATOA MSAADA WA MIFUKO 150 YA CEMENT KUBORESHA MADARASA
BIASHARA

TANZANIA COMMERCIAL BANK YAIPIGA JEKI SEKTA YA ELIMU YATOA MSAADA WA MIFUKO 150 YA CEMENT KUBORESHA MADARASA

by Ally Hamis Zingizi
Jan 27, 2023
TANZANIA COMMERCIAL BANK YATOA MSAADA WA MIFUKO 100 YA SARUJI KUKAMILISHA UJENZI WA ZAHANATI YA KATA YA GOWEKO
BIASHARA

TANZANIA COMMERCIAL BANK YATOA MSAADA WA MIFUKO 100 YA SARUJI KUKAMILISHA UJENZI WA ZAHANATI YA KATA YA GOWEKO

by Ally Hamis Zingizi
Jan 27, 2023
Benki ya NBC Yahitimisha Kampeni ya ‘Vuna Zaidi na NBC Shambani’
BIASHARA

Benki ya NBC Yahitimisha Kampeni ya ‘Vuna Zaidi na NBC Shambani’

by ALFRED MTEWELE
Jan 27, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
December 2022
M T W T F S S
 1234
567891011
12131415161718
19202122232425
262728293031  
« Nov   Jan »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In