ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Monday, January 30, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

DKT. MPANGO ATOA WITO KWA TBA KUZINGATIA UBORA

Dodoma, Tanzania

ALFRED MTEWELE by ALFRED MTEWELE
Dec 1, 2022
in HABARI
0
DKT. MPANGO ATOA WITO KWA TBA KUZINGATIA UBORA
0
SHARES
28
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

RelatedPosts

DKT. JAFO AHIMIZA WATANZANIA KUTUNZA MAZINGIRA

DKT. JAFO AHIMIZA WATANZANIA KUTUNZA MAZINGIRA

Jan 9, 2023

MAJI YA MVUA YATAKIWA KUVUNWA KUEPUSHA UHARIBIFU MAZINGIRA

Dec 15, 2022

Rais Samia Aihimiza Jamii Kupanda Miti Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi

Nov 24, 2022
Load More
May be an image of 9 people and people standing
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kuhakikisha Miradi ya Ujenzi wanayotekeleza inazingatia ubora, tija,gharama nafuu pamoja na ujenzi wa kisasa unaoendana na wakati ili miradi hiyo idumu kwa muda mrefu na kuwa na tija kwa wapangaji.
Makamu wa Rais amesema hayo tarehe 30 Novemba 2022 wakati wa Hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Mradi wa Ujenzi wa Nyumba 3,500 za Watumishi wa Umma zinazojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) katika eneo la Nzuguni Jijini Dodoma. Ameongeza kwamba ni vyema TBA kufanya mapinduzi makubwa ya kiutendaji, kuongeza ubunifu na kujenga misingi mizuri ya kujiendesha kibiashara ili kuweza kupata mapato zaidi na kujiendesha pasipo kutegemea ruzuku kutoka serikalini.
Aidha Makamu wa Rais ameitaka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kuharakisha mchakato wa marekebisho ya kanuni ya Uanzishwaji wa Wakala wa Nyumba Tanzania ili Taasisi iweze kukamilisha taratibu zote za kuingia ubia na wawekezaji hali itakayopunguza utegemezi wa ruzuku ya Serikali pekee katika kutekeleza miradi mikubwa nchini na pia itatatua changamoto ya kuchelewa kwa utekelezaji wa miradi hiyo.
Halikadhalika Makamu wa Rais amewataka TBA kuweka utaratibu shirikishi kwa lengo la kuimarisha ulinzi na usalama wa watu na mali zao katika maeneo ya nyumba hizo. Pia amewasihi Watumishi wa Umma watakaopangiwa nyumba hizo kuzitunza na kuhakikisha zinabaki katika hali ya ubora wake ikiwemo kuzingatia masuala ya usafi na utunzaji mazingira.
Makamu wa Rais amesema Uwekezaji katika Sekta ya ujenzi ni miongoni mwa vipaumbele muhimu vya Serikali ya Awamu ya Sita ambayo inaendelea kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kama ilivyopangwa. Aidha amesema Serikali itaendelea kuunga mkono ubunifu na mipango ya Taasisi kama TBA kuwa na miradi mingi zaidi ya ujenzi ili kuongeza makusanyo ya ndani na kupunguza utegemezi wa ruzuku kutoka Serikalini.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema mradi huo utapunguza changamoto kubwa ya makazi ya watumishi wa umma waliopo jijini Dodoma pamoja na ukuzalisha ajira kwa wananchi wanaozunguka mradi huo.
Profesa Mbarawa ameongeza kwamba ujenzi wa mradi huo unasaidia Wataalamu wazawa wa fani za ujenzi kujengewa uwezo wa taaluma kwa vitendo pamoja na kusaidia kuendelea kukua kwa kasi kwa jiji la Dodoma lililopangwa vizuri kwa kuzingatia mipango miji , kuongezeka kwa mapato ya serikali na huduma za kijamii katika jiji hilo.
Awali akitoa taarifa za ujenzi wa mradi huo, Mtendaji Mkuu wa TBA Arch. Daudi Kandoro amesema tayari serikali imetoa gharama za utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mradi huo kiasi cha shilingi bilioni 14.3 pamoja na kutoa shilingi bilioni 1 katika mwaka wa fedha 2022/23 kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi huo wa nyumba nyingine 150 ambapo maandalizi yake yameshaanza.
Kandoro Amesema TBA inaendelea kutekeleza miradi mingine nchi nzima kwa fedha za ruzuku na makusanyo ya ndani ikiwemo mradi wa ujenzi wa nyumba mpya 20 za Viongozi katika eneo la Kisasa Dodoma, ukamilishaji wa nyumba za majaji kwenye Mikoa ya Kilimanjaro, Mtwara, Shinyanga, Tabora na Kagera, ukarabati wa nyumba za makazi ya watumishi wa Umma na Viongozi Tanzania Bara ili kuwawezesha kuishi katika mazingira bora, Ujenzi wa nyumba za makazi kwa Watumishi wa Umma katika eneo la Magomeni Kota na Temeke Kota, Ujenzi wa jengo la makazi eneo la Masaki, ujenzi wa nyumba 13 za watumishi Mikoani, umaliziaji wa jengo la makazi la ghorofa 11 lenye uwezo wa kuchukua familia 22 Mtaa wa Simeoni Arusha.
May be an image of 12 people and people standing
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

Related

Tags: OFISI YA MAKAMU WA RAIS
ADVERTISEMENT
ALFRED MTEWELE

ALFRED MTEWELE

Related Posts

WIZARA YA AFYA YATOA FURSA KWA RAIA 12 KUSIMAMIA MIRADI
HABARI

WIZARA YA AFYA YATOA FURSA KWA RAIA 12 KUSIMAMIA MIRADI

by ALFRED MTEWELE
Jan 30, 2023
NMB kupeleka washindi 8 Dubai kupitia Droo ya ‘Grand Finale’
HABARI

NMB kupeleka washindi 8 Dubai kupitia Droo ya ‘Grand Finale’

by I am Krantz
Jan 30, 2023
Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti leo Ijumaa 25.11.2022
HABARI

Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti ya Leo Januari 30,2023

by ALFRED MTEWELE
Jan 30, 2023
WATU WENGI WALIJUA NITAVAA RANGI YA KINYOKA NYOKA – MANZOKI
HABARI

WATU WENGI WALIJUA NITAVAA RANGI YA KINYOKA NYOKA – MANZOKI

by Shabani Rapwi
Jan 29, 2023
SIMBA KUSHINDA UBINGWA MSIMU HUU
HABARI

SIMBA KUSHINDA UBINGWA MSIMU HUU

by Shabani Rapwi
Jan 29, 2023
WANAFUNZI WALIOMDHALILISHA MTANDAONI  MWANAFUNZI WA CHUO CHA CDTI WAKAMATWA
HABARI

WANAFUNZI WALIOMDHALILISHA MTANDAONI MWANAFUNZI WA CHUO CHA CDTI WAKAMATWA

by Shabani Rapwi
Jan 29, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
December 2022
M T W T F S S
 1234
567891011
12131415161718
19202122232425
262728293031  
« Nov   Jan »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In