
Baada ya mvutano wa muda mrefu hatimaye, Uongozi wa Geita Gold FC umefunguka kuachana na mchezaji aliyekuwa anakipiga mnamo klabu hio, George Mpole.
Kwa sasa nyota huyo yupo huru kuwaniwa na kikosi chochote kitachoona uwezekano wa kumsajili ili kuweza kuhudumu rasmi baada ya makubaliano.
“Leo Tarehe 7/12/2022 Tumefikia makubaliano ya kuachana na mshambuliaji wetu George Enock Mpole.
Uongozi umefikia hatua hii baada ya kuzungumza na mchezaji kwa kina na kufikia maridhiano hayo kwa maslahi mapana ya klabu na mchezaji mwenyewe” Umesema Uongozi wa Geita Gold FC




ADVERTISEMENT