Hatimaye Mchekeshaji maarufu kutokea nchini Kenya kupitia kuigiza Sauti ya Mtangazaji maarufu wa Kandanda Duniani Peter Drury, ambaye anafahamika kama Arap Uria amepata nafasi ya Kuonana ana kwa ana na Mtangazaji huyo akiwa ameenda kutembea nchini Qatar.
Arap Uria aliwahi funguka katika moja ya mahojiano kuwa alivutiwa sana na alipenda kuwa mtangazaji licha amekuwa Mwalimu na hakuweza kupata nafasi ya moja kwa moja kuwa Mtangazaji sasa anatumia kipaji chake hicho cha uchekeshaji ili kutimiza moja ya ndoto yake kubwa.
Aliweza andika ujumbe wa kutaka kukutana na Mtangazaji maarufu wa soka la mpira wa miguu Duniani ambaye Sauti yake imeweza sikika katika mechi nyingi zilizochezwa hapo awali.


Huu ndio Ujumbe wa Arap Uria uliomtaka Peter Drury kuweza kukutana nae akiwa ndani ya nchi ya Qatar ambako michuano ya Kombe la Dunia inaendelea.