ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Monday, February 6, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

MAJI YA MVUA YATAKIWA KUVUNWA KUEPUSHA UHARIBIFU MAZINGIRA

Dodoma, Tanzania

ALFRED MTEWELE by ALFRED MTEWELE
Dec 15, 2022
in HABARI
0
MAJI YA MVUA YATAKIWA KUVUNWA KUEPUSHA UHARIBIFU MAZINGIRA
0
SHARES
21
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

RelatedPosts

SERIKALI YATOA SIKU 7 KUEPUSHA UCHAFUZI WA MAZINGIRA KISA KELELE NA MITETEMO

SERIKALI YATOA SIKU 7 KUEPUSHA UCHAFUZI WA MAZINGIRA KISA KELELE NA MITETEMO

Feb 3, 2023

SERIKALI YAJITOKEZA KUZUIA NA KUPAMBANA NA BIASHARA HARAMU

Jan 31, 2023

DKT. JAFO AHIMIZA WATANZANIA KUTUNZA MAZINGIRA

Jan 9, 2023
Load More
May be an image of 5 people and people standing
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ameelekeza majengo yote ya Serikali yanayojengwa katika eneo la Mtumba jijini Dodoma kuwekewa mfumo wa kuvuna maji ya mvua ili kuepusha athari za kimazingira.
Ametoa maelekezo hayo alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya la Ofisi ya Makamu wa Rais katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma Desemba 13, 2022.
Amesema ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi huo ikiwemo utekelezaji wa maelekezo ya kuweka mifumo ya uvunaji maji ya mvua aliyotoa alipokagua ujenzi huo mwezi Juni mwaka huu.
Dkt. Jafo amesema kuwa kujengwa kwa mifumo ya kuvuna maji ya mvua kutasaidia yasiweze kutiririka ovyo na kusababisha mmomonyoko wa udongo hivyo kuharibu mazingira.
“Kwa kweli nimefarijika sana na mnavyoendelea na utekelezaji wa mradi huu wa ujenzi wa jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais nilipofanya ziara hapa nilitoa maelekezo na nimekuta mnayatekeleza maana mmejenga tanki hili la lita laki tano litakalopokea maji ya mvua,” amesema Dkt. Jafo.
Aidha, Waziri Jafo ametoa rai kwa mkandarasi anayejenga jengo hilo kumaliza kazi zilizobakia kwa wakati ili jengo hilo liweze kukamilika ndani ya muda uliobaki.
Awali akiwasilisha taarifa ya mradi huo Mhandisi wa SUMA JKT Sajidu Bwikizo amesema ujenzi wa mradi huo umefikia asilimia 50 kwa mujibu wa mpango ambapo umefikia hatua ya usukaji wa nondo na umwagaji wa zege hadi sakafu (floor) ya sita.
Pia, Msimamizi wa Mradi, Meja Benedict Meena ameahidi kuyafanyia kazi maelezo ya waziri kwa kuweka mafundi wa kutosha katika kila sakafu ili kazi hiyo ifanyike na kukamilika kwa wakati.
Ikumbukwe kuwa ujenzi wa jengo hilo unasimamiwa na Mshauri elekezi Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na kutekelezwa na Mkandarasi SUMA JKT.
May be an image of 3 people and outdoors
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

Related

Tags: OFISI YA MAKAMU WA RAIS
ADVERTISEMENT
ALFRED MTEWELE

ALFRED MTEWELE

Related Posts

DIAMOND KANILIPA MILIONI 17 VIDEO YA ZUWENA
HABARI

DIAMOND KANILIPA MILIONI 17 VIDEO YA ZUWENA

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023
VIJANA ACHENI KU-BET FANYENI KAZI – CHONGOLO
HABARI

VIJANA ACHENI KU-BET FANYENI KAZI – CHONGOLO

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023
RAIS WA ZAMANI WA PAKISTAN AFARIKI DUNIA
HABARI

RAIS WA ZAMANI WA PAKISTAN AFARIKI DUNIA

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023
IDADI YA WALIOFARIKI AJALI YA TANGA YAONGEZEKA HADI 20
HABARI

IDADI YA WALIOFARIKI AJALI YA TANGA YAONGEZEKA HADI 20

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023
MANGE KIMAMBI AMCHANA  HAJI MANARA ‘WE NI MTU MZIMA’
HABARI

MANGE KIMAMBI AMCHANA HAJI MANARA ‘WE NI MTU MZIMA’

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023
NAJUA UCHUNGU WA MTOTO SIWEZI – WOLPER
HABARI

NAJUA UCHUNGU WA MTOTO SIWEZI – WOLPER

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
December 2022
M T W T F S S
 1234
567891011
12131415161718
19202122232425
262728293031  
« Nov   Jan »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In