ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Monday, February 6, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

NMB YATWAA TUZO YA MWAJIRI BORA AFRIKA

I am Krantz by I am Krantz
Dec 22, 2022
in HABARI
0
NMB YATWAA TUZO YA MWAJIRI BORA AFRIKA
0
SHARES
28
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT
Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Bw. Filbert Mponzi akikabithiwa tuzo ya Mwajiri Bora Afrika kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Bi. Ruth Zaipuna na Afisa Mkuu Rasilimali Watu, Bw Emmanuel Akonaay kwenye hafla fupi ya kupokea tuzo hiyo ya “the Best Employer Brand – Africa”. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Masoko, Rahma Mwapachu na kushoto ni Mwakilishi kutoka Idara ya Rasilimali Watu, Pamela Deteba.

Kwa mara nyingine tena, Benki ya NMB imedhihirisha umahiri na ukubwa wake kiutendaji na kiundeshaji nchini baada yakufanikiwa kunyakuwa tuzo ya mwajiri bora barani Afrika – the Best Employer Brand Africa.
Ushindi huo mkubwa ulipatikana wiki jana mjini Port Louis huko Maurituis ambako NMB ilitunukiwa tuzo hiyo inayotambua umakini katika kuzingatia maslahi na maendeleo ya wafanyakazi na waandaaji wake ambao ni taasisi ya ajira ya Employer Branding Institute.
Akipokea nishani hiyo jana makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Bw Filbert Mponzi, alisema tuzo hiyo ya nne ya mwajiri bora mwaka huu, ni ushahidi mwingine wa jinsi taasisi hiyo kubwa ya fedha nchini inavyothamini wafanyakazi wake.
“Thamani ya wafanyakazi kwetu sisi NMB ni kubwa sana kwani wao ndiyo rasilimali inayoongoza na chanzo cha mafanikio yetu yote na tuzo mbalimbali ambazo tumekuwa tunazipata ,” Bw Mponzi alisema baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo na Afisa Mkuu Rasilimali Watu, Bw Emmanuel Akonaay.
Kiongozi huyo ambaye pia ni Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB aliongeza kuwa baada ya kuongoza karibu kwa kila kitu nchini, sasa wameanza kupata mafanikio barani Afrika.

RelatedPosts

DIAMOND KANILIPA MILIONI 17 VIDEO YA ZUWENA

DIAMOND KANILIPA MILIONI 17 VIDEO YA ZUWENA

Feb 5, 2023

VIJANA ACHENI KU-BET FANYENI KAZI – CHONGOLO

Feb 5, 2023

RAIS WA ZAMANI WA PAKISTAN AFARIKI DUNIA

Feb 5, 2023
Load More

 

ADVERTISEMENT

Hii inatokana na NMB kuzingatia matakwa ya msingi ya uongozi na uendeshaji taasisi hasa zile za fedha. Ushindi wa mwajiri bora, alifafanua, unatokana na NMB kutambua umuhimu wa rasilimali watu na kuwekeza katika maendeleo yake.
Mbali ya kuwa mwajiri bora, pia NMB ndiyo benki bora na kiongozi nchini. Mwaka huu tu, NMB imeweza kujikusanyia zaidi ya tuzo 20 za kimataifa ilizotunukiwa na majarida yanayoheshimika duniani kama vile World Economic Magazine, Global Brands Magazine, International Banker Awards na International Business Magazine. Mwezi jana, NMB alinyakua tuzo tatu za mwajiri mahiri kutoka kwa chama cha waajiri nchini (ATE) ikiwemo ile ya mwajiri bora wa mwaka 2022.
Bw Akonaay ambaye ndiye aliipokea tuzo ya Best Employer Brand – Africa huko Mauritius tarehe 13 mwezi huu alisema tuzo hiyo ni mwendelezo wa mambo makubwa ya NMB kwa mwaka huu.
Akizungumza kabla ya kuikabidhi rasmi kwa Bw Mponzi, mtaalamu huyo wa ajira na wafanyakazi alisema heshima waliyopata inazidi kuifanya NMB kutambulika barani Afrika na duniani kote kwa ujumla.
Kiongozi huyo aliongeza kuwa ushindi walioupata unatokana na juhudi za bodi na menejimenti ya NMB lakini zaidi wafanyakazi wa benki hiyo. NMB, alifafanua, imeonyesha kuwa si tu taasisi inayoongoza kwa huduma za kifedha bali pia ni kinara wa kujali maslahi ya wafanyakazi wake.
“Sisi tunaongoza si tu kwa biashara na huduma bora bali pia linapokuja swala la rasilimali watu,” alieleza.

ADVERTISEMENT

Related

ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

DIAMOND KANILIPA MILIONI 17 VIDEO YA ZUWENA
HABARI

DIAMOND KANILIPA MILIONI 17 VIDEO YA ZUWENA

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023
VIJANA ACHENI KU-BET FANYENI KAZI – CHONGOLO
HABARI

VIJANA ACHENI KU-BET FANYENI KAZI – CHONGOLO

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023
RAIS WA ZAMANI WA PAKISTAN AFARIKI DUNIA
HABARI

RAIS WA ZAMANI WA PAKISTAN AFARIKI DUNIA

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023
IDADI YA WALIOFARIKI AJALI YA TANGA YAONGEZEKA HADI 20
HABARI

IDADI YA WALIOFARIKI AJALI YA TANGA YAONGEZEKA HADI 20

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023
MANGE KIMAMBI AMCHANA  HAJI MANARA ‘WE NI MTU MZIMA’
HABARI

MANGE KIMAMBI AMCHANA HAJI MANARA ‘WE NI MTU MZIMA’

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023
NAJUA UCHUNGU WA MTOTO SIWEZI – WOLPER
HABARI

NAJUA UCHUNGU WA MTOTO SIWEZI – WOLPER

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
December 2022
M T W T F S S
 1234
567891011
12131415161718
19202122232425
262728293031  
« Nov   Jan »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In