Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC @salim_tryagain ameshiriki mafunzo kutoka FIFA kwa ajili ya Viongozi wa mpira duniani ambapo kwa Afrika wamechagua Viongozi watatu tuu kutoka klabu tatu Afrika.
Mafunzo hayo yanayoendelea nchini Qatar, Rais wa FIFA Gianni Infantino ni mmoja kati ya Wakufunzi, sambamba na Arsene Wenger na CEOs mbalimbali wa klabu za Ulaya, lengo ni kutoa darasa na kubadilishana uzoefu.
Wakufunzi wakuu ni CEO wa Manchester City, Ferran Soriano, Mwenyekiti wa Tottenham Dany Levy.
