ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Monday, February 6, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

VIONGOZI WATAKIWA KUIBEBA AJENDA YA UKATILI KWENYE VIKAO VYAO

Dar es Salaam, Tanzania

ALFRED MTEWELE by ALFRED MTEWELE
Dec 14, 2022
in HABARI
0
VIONGOZI WATAKIWA KUIBEBA AJENDA YA UKATILI KWENYE VIKAO VYAO
0
SHARES
23
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

RelatedPosts

SERIKALI YAJA  NA MBINU MBADALA  KUPAMBANA NA UKATILI

SERIKALI YAJA NA MBINU MBADALA KUPAMBANA NA UKATILI

Jan 26, 2023

SERIKALI YAFUTA MASHIRIKA 4898 YASIYO YA KISERIKALI

Jan 26, 2023

KATEKISTA ADAIWA KUBAKA MWANAFUNZI

Jan 24, 2023
Load More
May be an image of 13 people and people standing
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mh Dkt. Dorothy Gwajima ametoa wito kwa viongozi hasa wa Kata, Vijiji na Mitaa kuifanya Ajenda ya ukatili wa kijinsia na kwa watoto kuwa ya kudumu katika majukumu yao.
Waziri Dkt. Gwajima ametoa wito huo alipozungumza na wananchi wa Kata ya Chamazi, Wilaya ya Temeke, Mkoani Dar es salaam ambapo ameshiriki na wananchi hao kuhitimisha madhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia na kwa watoto yaliyofanyika kwenye Kata hiyo, Desemba 13, 2022.
Amefafanua kwamba viongozi wana wajibu wa kujadili na kutafuta ufumbuzi kuhusu masuala ya ukatili kama ilivyo kwa masuala mengine ya muhimu kwenye maeneo yao.
Aidha, ameupongeza uongozi wa Kata ya Chamazi chini ya uongozi wa Diwani wa Kata hiyo Mhe. John Gama, kwa kuwa wa kwanza nchini kutekeleza wito wa kuunganisha nguvu za wadau wote pasipo itikadi za kiimani wala kisiasa katika kujipanga kuimarisha mapambano.
“Ndiyo maana Kiongozi namba moja Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alisema suala la ajenda ya ukatili wa kijinsia, uwezeshaji kiuchumi tulibebe. Hivyo kila kiongozi wa kijamii huko aliko hahitaji kuandikiwa barua ya kutekeleza. Twendeni na Ajenda ya kijamii, twendeni tukayachambue haya mambo tujue tunaishi vipi” amesema Waziri Dkt Gwajima
Ameendelea kusisitiza kuwa bila kujadili Masuala ya kijamii, ukatili haiwezi kuisha. Hivyo amesisitiza mwaka 2023 uwe ni mwaka wa kufanya mapinduzi kwenye vipaumbele vya ajenda za vikao ngazi zote kuanzia mtaa/kata na Halmashauri hadi Taifa.
Waziri Gwajima amesisitiza kuwa, ajenda ya kutokomeza ukatili wa kijinsia na kwa watoto ikipewa kipaumbele sambamba na kutumika kwa haki ya kisheria ya Halmashauri kutunga sheria ndogo ni Dhahiri mambo mengi yanayochochea ukatili huu wa kijinsia na kwa watoto yanaenda kukoma.
Amehimiza kuwa, pamoja na kuhitimisha siku 16, za Kampeni hiyo inaanza Kampeni endelevu ya siku 365 hivyo, majeshi yote ya jamii ikiwemo SMAUJATA, SKAUTI, GIRLS GUIDE, Majukwaa ya Wanawake, Wajane, wenye Ulemavu, Vijana, Wazazi, Mabaraza ya Wazee na Watoto, Polisi Kata na Dawati la Jinsia, Wasaidizi wa Kisheria, Viongozi wa Dini, Mashirika yasiyo ya kiserikali, Watoa huduma za Tiba Asili na wengine kwa pamoja chini ya uongozi wa Kamati za MTAKUWWA wakaandae mpango kazi kulingana na mazingira yao kisha taarifa ya utekelezaji iwe inawasilishwa kwenye vikao vyote vya Halmashauri.
Ameongeza pia Halmashauri zione uwezekano wa kutunga sheria ndogo kudhibiti vichocheo vya ukatili huu kwani halmashauri hizo zinayo mamlaka hayo kisheria. Aidha, ametoa wito kila mmoja kuwajibika kwa sababu ufuatiliaji utafanyika ngazi zote.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Chamazi Dafrosa Peter akitoa taarifa ya utekelezaji ya Kata amebainisha kuwa, mwezi Januari hadi Desemba mwaka huu, kata hiyo kwa kushirikiana wadau imepokea mashauri ya ukatili wa watoto 58 yakiwemo ya kingono 12,ya kudhuru mwili 19, utumikishwaji majumbani na maeneo mengine 15 ambapo, mashauri 12 kati ya hayo ymeshughulikiwa, 6 yanaendelea mahakamani na 3 tayari yamepatiwa hukumu.
Kwa upande wake Mkuu wa Dawati la Jinsia kituo cha Polisi mkoa wa Temeke Meckridige Mwingira amesema
Dawati hilo linafanya kazi na asasi za Serikali na zisizo za Serikali kutoa elimu katika shule za msingi na sekondari katika kata 10 za Wilaya hiyo na kubainisha makosa yanayoripotiwa hasa ni ubakaji, ulawiti, shambulio ya aibu, kutekeleza familia, ukatili wa watoto, ukatili dhidi ya wanaume.
Naye mmoja wa wananchi aliyeshiriki hitimisho hilo amewaasa wazazi kukaa karibu na watoto wao pamoja na changamoto zote za shughuli za kiuchumi wanazokumbana nazo.
MWISHO
May be an image of 11 people, people standing, outdoors and text that says 'KATI MKOMBOZI MONTESSORI PRE AND PRIMARY SCHOOL "WATOTO TUSEME TUNAYOYAONA,TUNAYOYASIKIA TUNAYOYASIKIA NATUNAYOFANYIWA ILI KUTOKOMEZA UXATILI DHIDI YETU".'
May be an image of 6 people and people standing
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

Related

Tags: WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII
ADVERTISEMENT
ALFRED MTEWELE

ALFRED MTEWELE

Related Posts

DIAMOND KANILIPA MILIONI 17 VIDEO YA ZUWENA
HABARI

DIAMOND KANILIPA MILIONI 17 VIDEO YA ZUWENA

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023
VIJANA ACHENI KU-BET FANYENI KAZI – CHONGOLO
HABARI

VIJANA ACHENI KU-BET FANYENI KAZI – CHONGOLO

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023
RAIS WA ZAMANI WA PAKISTAN AFARIKI DUNIA
HABARI

RAIS WA ZAMANI WA PAKISTAN AFARIKI DUNIA

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023
IDADI YA WALIOFARIKI AJALI YA TANGA YAONGEZEKA HADI 20
HABARI

IDADI YA WALIOFARIKI AJALI YA TANGA YAONGEZEKA HADI 20

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023
MANGE KIMAMBI AMCHANA  HAJI MANARA ‘WE NI MTU MZIMA’
HABARI

MANGE KIMAMBI AMCHANA HAJI MANARA ‘WE NI MTU MZIMA’

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023
NAJUA UCHUNGU WA MTOTO SIWEZI – WOLPER
HABARI

NAJUA UCHUNGU WA MTOTO SIWEZI – WOLPER

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
December 2022
M T W T F S S
 1234
567891011
12131415161718
19202122232425
262728293031  
« Nov   Jan »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In