

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Tehama na operesheni za Benki ya Stanbic – Mussa Ally alisema; ‘’Tuna nia kubwa na kampeni yetu ya Stanbic Madawati Initative ambayo hadi sasa imechangia takribani madawati 1000 kwa shule mbalimbali nchin,i tangu ilipozinduliwa. Mchango huu leo ni mwendelezo wa jitihada zetu za kuitikia wito wa serikali wa kuchangia madawati kwa lengo la kumaliza kabisa uhaba wa madawati shuleni. Kupitia mchango huu, Benki ya Stanbic inachochea uundaji wa nguvu kazi ya baadaye ya nchi. Tutaendelea kujitolea kusaidia sekta ya elimu sio tu hapa Wilaya ya Bagamoyo, bali Tanzania nzima.’’
Naye Diwani wa kata ya Kerege Saidi Abdullah Ngatipura ameipongeza benki ya Stanbic kwa jitihada zao za kuendelea kusaidia sekta ya elimu na kuwataka wadau wengine kuunga mkono shule nyingine wilayani humo.
Akipokea msaada huo Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Kerege, Kasika Mateko Kasika alisema kuwa, kupitia msaada huo, wanafunzi wa shule hiyo watakuwa na mazingira bora ya kujifunzia, jambo ambalo anatarajia litaongeza ufaulu wao.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi wakuu wa wilaya na serikali za mitaa kutoka Wilaya ya Bagamoyo
MWISHO.