
Wakati Dunia ikielekea ukingoni katika maadhimisho ya Kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amebaini kutojipanga vizuri kwa baadhi ya watendaji katika kushughulikia vitendo vya ukatili hasa katika ngazi za mitaa na vijiji.
Akizungumza na baadhi ya wananchi katika kata ya Dakawa, Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro Desemba 3, 2022 wamemueleza kutopewa elimu kuhusu vitendo vya ukatili tangu kampeni hiyo imeanza tarehe 25 Novemba.
Wananchi hao wamedai kutoijua kamati ya ulinzi wa wanawake na watoto ya kata hiyo ambapo
Waziri Dkt. Gwajima amegundua pia haifuati mwongozo wa uendeshaji wake.
Kufuatia hali hiyo, Waziri Dkt. Gwajima ametoa maelekezo kwa Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya hiyo Sia kuhakikisha kamati hizo zinafuata mwongozo wa uanzishwaji na uendeshaji wake.
Aidha amemtaka kuhakikisha wananchi wanapewa elimu ya kutosha katika siku hizi za Kampeni na baada ya Kampeni kwa kushirikiana na wadau wote wanaohusika na kupinga ukatili wilayani humo.
Waziri Gwajima aliendelea kusisitiza wanaume kujitokeza kushiriki kampeni ya kupinga ukatili kwa nguvu zote.
MWISHO
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT