ADVERTISEMENT

Siku chache hapo nyuma Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Silent Ocean Ltd Ndg. Salaah Said Mohamed alitangaza donge nono (ahadi) lenye thamani ya Shilingi Milioni 20 kwa Klabu inayoidhamini, Tanzania Prisons FC yaani endapo ikishinda dhidi ya Yanga itaweza jinyakulia kitita chote ila ikitoa droo itapewa Shilingi milioni 10.
Baada ya mchezo wa jana Kukamilika Yanga iliibuka na Ushindi wa Goli 1-0 lililofungwa na mchezaji wake Feisal Salum katika kipindi cha pili ndani ya Dakika ya 89′ na kufanya klabu ya Tanzania Prisons kupoteza kabisa bahati ya kujinyakulia kitita hicho hata nusu yake.
Kupitia kurasa za mitandao ya kijamii ya kampuni hio imefunguka kuwa haikuwa nafasi ya Klabu ya Tanzania Prisons FC kupata ushindi dhidi ya Yanga katika Michuano ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara licha ya kuwa walijitahidi kujituma.


“Haikua bahati ya 𝗪𝗔𝗝𝗘𝗟𝗔𝗝𝗘𝗟𝗔 𝗢𝗥𝗜𝗚𝗜𝗡𝗔𝗟 usiku wa leo kwa goli la dakika za mwisho kabisa. Tusikate tamaa tuendeleze mapambano.
Salamu kwa wachezaji wetu wote walioiwakilisha vyema nembo ya #simbawabahari
“


ADVERTISEMENT