Watu wanne wamefariki katika ajali iliyohusisha magari mawili hapo jana moja lenye namba za usajili T.162 DGN aina ya Toyota Spacio ikitokea Dodoma Kuelekea Dar es salaam na Lori lenye namba za usajili T. 654 DDN lililokuwa linatokea Jijini Dar es salaam kuelekea Dodoma baada ya kugongana uso Kwa uso katika eneo la Kwambe Barabara kuu ya Morogoro – Dodoma.
RPC wa Morogoro Alex Mukama ameripoti kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa mbili asubuhi, chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa Dereva wa gari dogo kutaka kuyapita magari yaliyopo mbele yake bila kuchukua tahadhari “Waliofariki wote ni waliokuwa kwenye gari dogo akiwemo Dereva ambaye nae amefariki”
Miili ya Marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya St. Joseph Dumila Wilayani Kilosa Kwa ajili ya utambuzi zaidi.
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT