Mfanyabiashara wa Saudi Arabia, Mushref al-Ghamdi amelipa zaidi ya Paundi milioni 2 ambayo ni zaidi ya Bilioni 6 na Milioni 344 kwa pesa ya Tanzania kununua tiketi ya VIP kushuhudia mchezo wa Kirafiki utakao wakutanisha Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.
ADVERTISEMENT
Mechi ya Alhamisi mjini Riyadh inatazamiwa kuwakutanisha Messi ya Paris Saint-Germain dhidi ya timu iliyochaguliwa inayoundwa na wachezaji wa klabu mpya ya Ronaldo ya Al Nassr na wapinzani wao wa Saudi Al Hilal.
ADVERTISEMENT