ADVERTISEMENT
Zao la nazi linatajwa kupanda bei maradufu kutokana na mvua kunyesha kwa uchache msimu uliopita wa mwaka 2022 hali inayopelekea watumiaji wa nazi hasa kwa mikoa ya Pwani kushindwa kumudu gharama zake.
Hivyo kutokana na kadhia hii ya mfumuko wa bei kwa aina ya bidhaa hio Mamlaka ya Hali ya Hewa, wizara ya Kilimo, Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Sekta ya kulinda Misitu wanahitaji kuwa na ushirikiano wa karibu ili kuweza kuweka ukomo wa suala hili mapema kwa miaka ijayo kwa kuendana na Mabadiliko ya Tabianchi.
ADVERTISEMENT