
Benki ya CRDB imeshiriki vilivyo katika uzinduzi wa mfuko wa uwekezaji wa pamoja “FAIDA FUND” wa shirika la @watumishi_housing_investments ambao unatoa fursa ya uwekezaji wa muda mfupi kwa makundi yote ya wananchi kukuza mitaji yao kwa faida nzuri.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo ya uzinduzi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama (ambaye alizitaka taasisi zinazohusika na mandeleo ya vijana, wanawake na makundi maalum kuhamasisha makundi hayo kuwekeza kwenye mfuko huo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema benki inajivunia kushiriki mchakato katika uanzishwaji wa mfuko huo. Nsekela alimuahidi Waziri Mhagama kuwa Benki ya CRDB kama msimamizi wa mfuko huo itahakikisha inatoa elimu ya kutosha ya uwekezaji ili wananchi wengi zaidi waweze kunufaika na fursa hiyo.
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT