
Benki ya NBC Yahitimisha Kampeni ya ‘Vuna Zaidi na NBC Shambani’, Yakabidhi Zawadi ya Trekta Kwa Wakulima wa Korosho Mtwara.
Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imetoa zawadi mbalimbali zikiwemo baiskeli, pikipiki na trekta kwa washindi wa mpango wa pili wa kampeni ya ‘Vuna Zaidi na NBC Shambani’ inayohusisha mkoa wa Mtwara.
Kampeni hii inalenga kuchochea kiwango cha uzalishaji wa zao la korosho na mazao mengine katika mkoa wa Mtwara.
Akizungumza mkoani Mtwara wakati wa hafla fupi ya kuhitimsha kampeni hiyo sambamba na kukabidhi zawadi kwa washindi wa kampeni hiyo ikiwemo zawadi kubwa ya trekta kwa Chama Kikuu cha Ushirika cha Masasi Mtwara (MAMCU), Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas alisema zawadi hizo zimekuja wakati muafaka kwa kuwa mkoa huo kwasasa unatekeleza mkakati wa kuongeza uzalishaji wa korosho kutoka tani 400,000 za sasa hadi tani 700,000 ifikapo mwaka 2025.
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT