ADVERTISEMENT
Chelsea wameweka dau la euro 120m (£105.6m) kumnunua kiungo wa kati wa Benfica na Argentina Enzo Fernandez katika hatua ambayo itamfanya kuvunja rekodi ya usajili ya Uingereza.
Kufikia sasa hakuna dalili kama ofa ya The Blues, inayofikiriwa kujumuisha malipo kwa awamu, itakubaliwa.
Lakini endapo dili hilo litakamilika, litapita kiasi cha £100m ambacho Manchester City walilipa Aston Villa kumnunua Jack Grealish mnamo 2021.
Fernandez alichaguliwa kuwa mchezaji chipukizi bora wa michuano hiyo wakati Argentina ilipotwaa ubingwa wa Kombe la Dunia nchini Qatar.
ADVERTISEMENT