Kiungo mkabaji, Danai Bhobho raia wa Zimbabwe amerejea tena katika kikosi cha timu ya Simba Queens na kusaini mkataba wa miaka miwili akitokea Harare City ya Zimbabwe.
–
ADVERTISEMENT
Danai alikuwepo kwenye kikosi cha Simba Queens kilichotwaa ubingwa wa Ligi kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite Women’s Premier League msimu wa 2020/21.
ADVERTISEMENT
–
Pia Danai alikuwepo katika kikosi cha Simba Queens kilichoshiriki Michuano ya CECAFA SAMIA CUP iliyofanyika nchini Kenya mwaka 2021. Danai anaungana na Mwanahamis Omary’Gaucho na Asha Rashid’ mwalala’ waliosajiliwa katika Dirisha Dogo kuongeza nguvu kikosini hapo.