
Dkt. Msonde ameyasema hayo leo Januari 19, 2023 Jijini Mwanza kwenye kikao kazi cha mapitio ya tathmini ya utekelezaji wa shughuli za uboreshaji na usimamizi wa elimu nchini.
Amesema imefika mahali viongozi wakatambua umuhimu wa kutoa motisha kwa walimu kwa kuwa ndio waliobeba dhamana ya malezi na ufundishaji wa watoto ambao ndio tegemeo la taifa.
Dkt. Msonde amesema mwalimu ni mzazi wa pili kwa kuwa anakaa na watoto wakiwa na umri mdogo mpaka wanapokuwa hivyo ni watu muhimu katika jamii ni wajibu wa viongozi kuwatunza kuwaheshimu na kuwadhamini.
“Walimu wanawajibu wa kuhakikisha nidhamu, maadili, uzalendo na utanzania wa mtoto unafundishwa na kushawishi jamii juu ya jinsi gani mtoto awe, hivyo ni vyema tukatoa motisha kwa walimu nchini ili kuongeza ari ya utunzaji na ufundishaji wa watoto wetu,”amesema Dkt. Msonde
Aidha, Dkt. Msonde ametumia fursa hiyo kutoa rai kwa walimu wote nchini kujitoa kwa moyo kwenye ufundishaji wa watoto kuanzia ngazi ya awali kwa kuwa ndio wamebeba dhamana ya kumkuza mtoto kimaadili, kiujuzi na kuhakikisha anajitegemea na kuwa raia mwema.

ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT