ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Friday, December 1, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

DODOMA WAPONGEZWA KWA KUPIGA HATUA KWENYE ELIMU

Dodoma

MTEWELE ALFRED by MTEWELE ALFRED
Jan 23, 2023
in HABARI
0
DODOMA WAPONGEZWA KWA KUPIGA HATUA KWENYE ELIMU
0
SHARES
44
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
May be an image of 4 people and people standingMAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Philip Isdori Mpango amesema, Mkoa wa Dodoma wamepiga hatua kubwa kwenye ufaulu nchini.
Hayo yamesemwa Januari 20, 2023 kupitia hotuba ya Makamu wa Rais iliyosomwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe.Angellah Kairuki (Mb) katika hafla ya kuufahamisha umma mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita katika Mkoa wa Dodoma.
“Katika eneo la elimu, Mkoa wa Dodoma mmepiga hatua kubwa kwenye ufaulu. Taarifa za Baraza la Mitihani kuhusu ufaulu wa darasa la saba, zinaonesha kuwa Mkoa wa Dodoma uko katika kumi bora kwa ufaulu kitaifa na kwa mara ya kwanza Halmashauri ya Wilaya Bahi imeingia katika halmshauri kumi bora kitaifa.
“Nisisitize kuwa, Mkoa wa Dodoma una nafasi ya kufanya vizuri zaidi. Tuhamasishe upatikanaji wa chakula mashuleni ili wanafunzi wetu watulie na kusoma vizuri,”amesema.
Pia ametaka walimu kupewa ushirikiano, kwani wanafanya kazi kubwa ya kuliandaa taifa la kesho na kuwapa motisha kila wanapofanya vizuri.
“Motisha wapewe sio kwa wale wanaofanya vizuri kitaifa tu, bali hata wale wanaofanya vizuri kimkoa, kiwilaya, na hata katika kata. Serikali itaendelea kuwekakipaumbele cha juu kwa sekta ya Elimu ili watoto wetu wawe Watanzania bora wanaoipenda nchi yao.
“Hapa, nitoe wito kwa kila mzazi kuhakikisha watoto wanaoingia darasa la awali, darasa la kwanza, na kidato cha kwanza wanaripoti shuleni,”amesema Waziri Kairuki kwa niaba ya Makamu wa Rais.
Amesema, Serikali imefanya jitihada kubwa kuboresha miundombinu ya elimu na kuajiri waalimu kwa kiasi kikubwa. “Furaha ya Mheshimiwa Rais wetu ni kuona kila mtoto anaypaswa kusoma yuko shuleni, darasani.
“Tukitekeleza hilo, tutakuwa tumempatia Mhe.Rais malipo tuliyopaswa kumlipa. Niwasihi pia wazazi wote, washiriki katika mikakati mbalimbali na program za kuboresha elimu katika mikoa yenu.
“Ninawata viongozi wa mkoa kutumia fursa ya uwepo wa vyuo vikuu na vyuo vya elimu vilivyoko katika mkoa wa Dodoma kuboresha huduma za kufundisha watoto wetu,”amesisitiza Makamu wa Rais kupitia hotuba iliyosomwa na Waziri Kairuki.
May be an image of 2 people, people standing and indoor
May be an image of one or more people, people sitting and people standing
ADVERTISEMENT

Related

Tags: OFISI YA RAIS TAMISEMI
ADVERTISEMENT
MTEWELE ALFRED

MTEWELE ALFRED

Related Posts

Tuliishi maisha ya shida sana kisa uchawi wa jirani!
HABARI

Tuliishi maisha ya shida sana kisa uchawi wa jirani!

by I am Krantz
Nov 30, 2023
EACOP Yakamilisha Utaratibu Wa Fidia Kwa Kukabidhi Nyumba Ya 339 Mkoani Tanga
HABARI

EACOP Yakamilisha Utaratibu Wa Fidia Kwa Kukabidhi Nyumba Ya 339 Mkoani Tanga

by I am Krantz
Nov 29, 2023
MAWAKALA WA USAJILI WA VODACOM TANZANIA WATEMBELEA AFRIKA YA KUSINI KUTOKANA NA UTENDAJI BORA WA KAZI.
HABARI

MAWAKALA WA USAJILI WA VODACOM TANZANIA WATEMBELEA AFRIKA YA KUSINI KUTOKANA NA UTENDAJI BORA WA KAZI.

by I am Krantz
Nov 29, 2023
NMB, Oryx Tanzania wazindua ‘Moto Mkali Bei Poa,’ kukopesha gesi ya kupikia
HABARI

NMB, Oryx Tanzania wazindua ‘Moto Mkali Bei Poa,’ kukopesha gesi ya kupikia

by I am Krantz
Nov 27, 2023
Kampeni Ya Serengeti Maokoto Ndani Ya Kizibo Yazidi Kusambaza Furaha Kwa Watanzania
HABARI

Kampeni Ya Serengeti Maokoto Ndani Ya Kizibo Yazidi Kusambaza Furaha Kwa Watanzania

by I am Krantz
Nov 27, 2023
NMB Mlipa Kodi Mkubwa na Bora Zaidi Tanzania 2023 🇹🇿
HABARI

NMB Mlipa Kodi Mkubwa na Bora Zaidi Tanzania 2023 🇹🇿

by I am Krantz
Nov 27, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TWEETS

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
January 2023
M T W T F S S
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031  
« Dec   Feb »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In