ADVERTISEMENT
Aliyewahi kukaimu nafasi ya Afisa habari na mawasiliano Simba SC, Ezekiel Kamwaga ametuma ujumbe kwa Masau Bwire unaohisiana kuacha kuizungumzia Klabu ya Simba kwa kuifananisha ubora wake na vilabu vingine barani Afrika..
MASSAU BWIRE “Wakati mnaijadili Simba Kama mwana Simba ujue haya yafuatayo::
1: Simba kwa hapa Africa inazidiwa ubora na timu 11 tu. Zingine zooote unazozijua wewe zipo chini ya Simba kwa ubora, ukikutana na shabiki anaibeza Simba mwambie kwa msisitizo kwamba Africa yote Simba inazidiwa ubora na timu 11 tu. Akisema zitaje usihofu tiririka tu.
Misri Simba inazidiwa ubora na timu 3 ambazo ni.
1: Al ahily
2: Zamaleki na
3: Pyramids
Nyingne zote unazijua misri zimepitwa na Simba kwa ubora.
Morocco ambao wamecheza kombe la dunia juzi tu Kuna timu 3 zinazoizidi Simba ubora nazo ni:
1: Wydad
2: Raja na
3: Barkane
Zingine zote unazozijua pale Morocco zipo chini ya Simba kwa ubora.
Tunisia ni timu 1 tu nayo ni:
1: Explence the Tunis
Zingine zote unazozijua pale Tunisia zipo chini ya Simba kwa ubora.
South Africa ni 1 tu nayo ni,
1:Mamelod Sundown
Algeria ni timu 1 tu nayo ni,
1: CR Belauzadad
Zingine zote unazozijua pale Algeria zipo chini ya Simba kwa ubora.
Angola ni moja tu nayo ni:
1: Petro Atletico
Zingine zote unazozijua pale zipo chini ya Simba kwa ubora.
Mwisho Congo ni Mazembe tu zingine zote unazozijua pale zipo chini ya SIMBA kwa ubora Africa.
Nchi nyingne zote unazozijua Africa, hakuna timu yenye ubora kama wa Simba, na hii siyo mtazamo wangu wala wako ni CAF wenyewe wenye timu zao Africa ndo wameweka hizo rank.
mwenye Povu lolote mwambie apeleke CAF

lakini ukweli lazima tuuseme.




ADVERTISEMENT