ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Monday, January 30, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

HUDUMA YA KUJIPIMA VVU MAHALA PA KAZI YAANZA

Dodoma

ALFRED MTEWELE by ALFRED MTEWELE
Jan 13, 2023
in HABARI
0
HUDUMA YA KUJIPIMA VVU MAHALA PA KAZI YAANZA
0
SHARES
16
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

RelatedPosts

WIZARA YA AFYA YATOA FURSA KWA RAIA 12 KUSIMAMIA MIRADI

WIZARA YA AFYA YATOA FURSA KWA RAIA 12 KUSIMAMIA MIRADI

Jan 30, 2023

BILIONI 1.3 ZATENGWA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA KATA YA ORKOLILI

Jan 24, 2023

WAZIRI UMMY AENDELEA KUSISITIZA UMUHIMU WA BIMA YA AFYA

Jan 23, 2023
Load More
May be an image of 11 people, people standing, people sitting and indoorSERIKALI kupitia Wizara ya Afya imeanzisha huduma ya kujipima VVU mahala pa kazi ili kurahisisha upatikanaji wa huduma ya vipimo vya VVU kwa watumishi makazini hasa wanaume, ambapo hadi kufikia Desemba 2022 watu wapatao 96,231 wamepatiwa huduma ya JIPIME mahala pa kazi.
Hayo yamejiri leo Januari 13, 2023, Jijini Dodoma wakati wakati Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel akiwasilisha taarifa kuhusu kuhuisha na kujumuisha maswala ya UKIMWI mbele ya kamati ya kudumu ya Bunge ya masuala ya UKIMWI.
“Wizara imeanzisha huduma ya kujipima VVU (JIPIME) mahala pa kazi ili kurahisisha upatikanaji wa huduma ya vipimo vya VVU kwa watumishi sehemu za kazi hususani Wanaume. Hadi kufikia Desemba 2022 watu wapatao 96,231 wamepatiwa huduma ya JIPIME mahala pa kazi.” amesema Dkt. Mollel.
Sambamba na hilo amesema, hadi kufikia Desemba 2022 jumla ya vijana balehe 47,705 (Wavulana 20,329 na Wasichana 27,376) walifikiwa katika shule zipatazo 103 kupitia kampeni ya Kipepeo, huku akibainisha kuwa, Kampeni hii inatarajiwa kufanyika mwaka 2023 katika mikoa ya Dodoma, Singida, Morogoro, Tanga na Geita.
Ameendelea kusema kuwa, kwa mwaka 2022 Wizara kwa kushirikiana na TACAIDS na Wizara ya Elimu imeweza kutoa mafunzo ya elimu ya jinsia kwa walimu wapatao 5,033 nchini.
Pamoja na hayo, Dkt. Mollel amesema, hadi kufikia Desemba 2022 kuna vituo vitano (5) vya kutolea huduma za afya katika maeneo ya Geita Gold Mine (Geita), North Mara Gold Mine (Mara), Bulyanhulu Gold Mine Limited (Shinyanga), New Luika Gold Mine (Songwe) na Mererani (Manyara).
Amesema, huduma za VVU zinazotolewa katika migodi hiyo ni pamoja na Upimaji wa VVU, huduma za tiba na matunzo ikiwemo utoaji wa ARV, huduma za tohara, huduma za JIPIME, huduma za dawa kinga (PrEP) na magonjwa mengine ya ngono.
Kwa upande wa wakazi wanaokaa maeneo yasiyifikika kwa urahisi hususani visiwani, amesema, Wizara imekuwa ikitoa huduma za VVU na UKIMWI kwa njia ya huduma mkoba ngazi ya jamii na baadhi ya maeneo kama visiwa hususani Ziwa Vitoria Mkoani Mwanza huduma hii hutolewa kwa kutumia usafiri wa boti maalum (Fikia boat).
Aidha, Dkt. Mollel amesema, Kwa kipindi cha Januari hadi Desemba 2022 jumla ya kondomu 111,934,600 zilisambazwa nchini ili kuongeza mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI, huku kati ya hizo, kondomu 2,806,500 zimesambazwa katika Wizara na Taasisi mbalimbali.
Mwisho.
May be an image of 2 people, people sitting and people standing
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

Related

Tags: Wizara ya Afya
ADVERTISEMENT
ALFRED MTEWELE

ALFRED MTEWELE

Related Posts

WIZARA YA AFYA YATOA FURSA KWA RAIA 12 KUSIMAMIA MIRADI
HABARI

WIZARA YA AFYA YATOA FURSA KWA RAIA 12 KUSIMAMIA MIRADI

by ALFRED MTEWELE
Jan 30, 2023
NMB kupeleka washindi 8 Dubai kupitia Droo ya ‘Grand Finale’
HABARI

NMB kupeleka washindi 8 Dubai kupitia Droo ya ‘Grand Finale’

by I am Krantz
Jan 30, 2023
Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti leo Ijumaa 25.11.2022
HABARI

Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti ya Leo Januari 30,2023

by ALFRED MTEWELE
Jan 30, 2023
WATU WENGI WALIJUA NITAVAA RANGI YA KINYOKA NYOKA – MANZOKI
HABARI

WATU WENGI WALIJUA NITAVAA RANGI YA KINYOKA NYOKA – MANZOKI

by Shabani Rapwi
Jan 29, 2023
SIMBA KUSHINDA UBINGWA MSIMU HUU
HABARI

SIMBA KUSHINDA UBINGWA MSIMU HUU

by Shabani Rapwi
Jan 29, 2023
WANAFUNZI WALIOMDHALILISHA MTANDAONI  MWANAFUNZI WA CHUO CHA CDTI WAKAMATWA
HABARI

WANAFUNZI WALIOMDHALILISHA MTANDAONI MWANAFUNZI WA CHUO CHA CDTI WAKAMATWA

by Shabani Rapwi
Jan 29, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
January 2023
M T W T F S S
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031  
« Dec    
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In