&

Kampuni ya inDrive imeanza rasmi shughuli zake jijini Dar es Salaam, ambalo ndilo jiji kubwa zaidi nchini Tanzania. Sasa, unaweza kuagiza gari kwa safari zote za kuzunguka jiji na maeneo yanayozunguka jiji kwa bei nafuu. Huduma hii imekuwepo Tanzania tangu mwaka wa 2018 na umekuwa na mafanikio makubwa.
inDrive, ambalo ni jukwa la Tehama la kimataifa linalofanikisha usafiri na huduma mbali linaanza shughui zake jijini Dar es Saaam.inDriver imekuwa ikiwashughulikia watu kwa mafanikio nchini Tanzania tangu 2018, ikitoa huduma za mjini, miunganisho na usafirishaji kwa Watanzania wanaoishi humo. Kutokana na mafanikio makubwa yaliyoshuhudiwa katika majiji ya mataifa mengine, kampuni ya inDriver ina matarajio kuwa wakazi wa Dar es Salaam wanahitaji sana huduma hiyo.
Inavyofanya Kazi
Kipengele cha inDrive chenye utofauti ni kuwa abiria na dereva kwa pamoja wanaweza kuwa na makubaliano moja kwa moja kuhusu gharama na maelezo mengine ya safari. Makubaliano hayo kamwe hayatabadilika kwa sababu zinazohusiana na umbali, msongamano wa magari mjini au hata hali ya hewa.
Watumiaji wote wa inDrive wana uhuru wa kufanya maamuzi au wa kuchagua. Abiria wanaweza kuchagua madereva kwa ukadiriaji, kwa chapa ya gari, miongoni mwa vigezo vingine muhimu.
Vile vile, madereva pia wanaweza kuchagua huduma za kujibu. Chaguo la hawa madereva linategemea bei inayotolewa na abiria tofauti, njia itakayotumika, umbali wa safari na ukadiriaji wa abiria.Wakiridhika na vigezo vyote isipokuwa bei, wanaweza kuwasilisha ofa mbadala.
Wakaazi wa jiji la Dar es Salaam wataweza kupata huduma hizi kwa njia ya gari au boda boda.
Evgeny Kalinin, Meneja wa Maendeleo ya Biashara Afrika: “inDrive, kila mara hufuata kanuni zake za kuchangia maendeleo duniani kupitia teknologia mpya. Ni muhimu sana kwetu kutoa mchango kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi yoyote tunayofanyia kazi. Tunatii kanuni mbali mbali za nchi kikamilifu kwa hivyo Tanzania, tuna leseni rasmi kutoka LATRA. Tunaunga mkono kikamilifu udhibiti wa serikali kwenye swala la utoaji wa leseni, na vizuizi vinavyohusisha utoaji huo na tume sio kikwazo kwetu. inDriver ina mipango ya kuongeza uwepo wake nchini Tanzania na iko tayari kukidhi mahitaji ya usafiri ya ndani ya miji tofauti na ya usafiri kati ya miji tofauti.”

Maelezo ya malipo
Huduma zote hulipwa kwa pesa taslimu na malipo yote hufanywa moja kwa moja kati ya wanaotumia huduma. inDrive haiwatozi madereva ada za kamisheni kwa sasa mjini Dar es Salaam, na tutakapoanza, ada haitazidi 10% ya thamani ya huduma iliyotolewa. Hii ni asilmia ya chini sana ukilinganisha na tozo zinazotolewa na washindani wetu.
Usalama
inDrive ina leseni rasmi ya LATRA (Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu nchini Tanzania).
Mfumo wa usalama wa inDriver umejengwa juu ya kanuni zinazotumiwa na wahusika wakuu wa sekta. Mbali na mfumo unaokubalika kwa ujumla wa hakiki na ukadiriaji wa watumiaji wa pande zote mbili, kampuni hukusanya aina nyingine ya data (ikiwemo uthibitishaji wa watumiaji kwa nambari za simu), ambayo ikilazimika, inaweza kutolewa kwa mashirika ya utekelezaji wa sheria.
Kuhusu inDrive
inDrive ilianzishwa mwaka wa 2013 ili kuwapa watumiaji njia mbadala yenye sera za bei zisizobadilika na zinazofaa kuwaepusha na huduma za kawaida za teksi ambazo hubadilisha bei iliyokuwepo awali kutegemea vipengele tofauti vya safari. Huduma hii hufanya kazi kwa kuzingatia kanuni ya kipekee ya uwekaji bei ambayo inawaruhusu abiria na dereva kujadiliana moja kwa moja kuhusu nauli. Hii inahakikisha kuwa masharti yanabakia wazi na ya haki.
Kufikia leo, inDrive ndiyo huduma ya uagizaji magari mtandaoni inayokua kwa kasi zaidi duniani. Programu yake imepakuliwa zaidi ya mara milioni 150. Huduma hiyo inapatikana katika miji zaidi ya 645 na nchi 45. Makao yake makuu yanapatikana katika eneo la Mountain View, California. Ina vitovu vya kikanda kule Amerika, Asia, Mashariki ya Kati, Afrika na nchi za CIS na pia huajiri zaidi ya watu 2,000 ulimwenguni.
Mapema 2021, inDrive ilipata hadhi ya unicorn baada ya kufunga awamu ya uwekezaji ya $150m na Insight Partners, General Catalyst, na Bond Capital, ambayo iliiwekea kampuni hiyo thamani ya $1.23 bilioni.
inDrive huendeleza operesheni zake ikiwa imejitolea kutekeleza kanuni ya uhuru wa kuchagua katika maeneo yake mengine ya biashara pia. Kwa hivyo, unaweza pia kuitumia jukwaa lake moja kwa utafutaji wa wasafirishaji, wataalamu wenye ujuzi, wabunifu mbalimbali na wakufunzi kufanya safari za mbali, kuhifadhi usafirishaji wa mizigo, au kupata huduma zingine (huduma zingine zinaanzishwa na kuongezwa hatua kwa hatua katika miji ambayo ina inDrive)