Mchezaji mahiri mwenye asili ya chini Congo anayekipiga mnamo klabu ya Singida Big Stars, Kazadi Kasengu amedhihirisha kwa mara nyingine ubora wake wa kupachika mabao kwa namna isiyotarajiwa.
kwani katika mchezo wao dhidi ya Azam FC wakiwa wanawania nafasi ya Ushindi wa Kombe la Mapinduzi huko Visiwani Zanzibar ameifanya timu yake iweze kuibuka na ushindi wa goli 4 -1 (goli zote nne zimewekwa kimiani na nyota huyo) hadi kupelekea mpinzani wake kutolewa katika muendelezo wa kuwania Kombe hilo.
Nyota huyo amewahi pia kuvisumbua vikosi vya Simba SC na Yanga SC kwa kupachika aina hiyo ya magoli yasiotarajiwa kufungwa kwani kwa upande wake hutumia nafasi za makosa machache ya mpinzani ili kumuadhibu vikali.