Mchungaji Dkt Eliona Kimaro aliyekuwa akihudumu katika kanisa la Kiinjiristi KKT la Kilutheri Kijitonyama apewa likizo ya Siku 60 kupitia Uongozi wa Makao makuu, hivyo anatakiwa kurejea na kuripoti Machi 17, 2023 kwa mujibu wa maelekezo kutoka kwenye barua aliyopewa.
Mchungaji huyo aliagana na waumini wa Kanisa hilo kwa masikitiko makubwa kwa kumuachia kijiti Mchungaji Ana katika kuendeleza kuratibu taratibu na kutoa huduma zote zihusianazo na ibada kwa kipindi ambacho yeye hatakuwepo.
Hata hivyo katika kurejerea barua aliopewa inaonyesha kuwa anatakiwa kuripoti kwa Ofisi za makao makuu ambako pia hatoweza tena kurejea katika kanisa hilo bali atapangiwa mahala pengine pa kuhudumu pale likizo yake ikiwa imetamatika.