Rais wa Zambia Hakainde Hichilema amesema ili kupunguza idadi ya talaka nchini humu lazima raia wa nchi hiyo waache kuchunguza simu za wapenzi wao
–
Rekodi zinaonyesha kuwa nchi ya Zambia ilirekodi zaidi ya kesi 22,000 za talaka mwaka jana pekee, takwimu ambazo Rais Hichilema alizitaja kuwa za kusikitisha
–
Inaelezwa kuwa pamoja na sababu kadhaa ikiwemo Ukosefu wa haki za ndoa, uzinzi, unyanyasaji wa kijinsia kuchangia ongezeko la talaka lakini pia suala la wapenzi kuchunguzana simu zao linachangia talaka nyingi nchini humo
–
“Tunaoana kwa ajili ya mapenzi, hatuoi ili kwenda kuangaliana, au kwenda kunyoosheana kidole,” amesema Rais Hichilema
–
Takwimu za miezi 12 iliyopita zilionyesha ndoa fupi zaidi nchini humo ilidumu kwa siku 30 huku ndefu zaidi ikiwa ni miaka 65