Muigizaji wa filamu ambaye kwa hivi sasa anafanya vizuri sana kupitia filamu za Kibongo na video vixen, Careen Simba amesema anawachukia wanaume ambao hawawapi fedha wapenzi wao wala hawawajali na kuwahudumia.
–
Ameongeza kuwa jukumu la mwanaume siku zote ni kumpa fedha mpenzi wake na anavyompa si kama anamhonga bali ni kumlinda na kumhudumia. “Hakuna kitu ninachochukia kama mwanaume kuona kuwa kumpa pesa mwanamke ni kumhonga wakati ni jukumu lake.
–
“Kama ni mwanamke wako lazima umhudumie ingawa na yeye anatakiwa
afanye kazi, siyo kila kitu mpaka amwambie
mwanaume wake,” amesema.
–
Amesema kuwa siku zote anaamini kuwa mwanamke kama utajitambua mwenyewe na kujiheshimu hakuna mwanaume au mtu yeyote anayeweza kukusumbua.
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT