ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Monday, February 6, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

NMB YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA HOSPITALI YA MICHEWENI PEMBA

I am Krantz by I am Krantz
Jan 4, 2023
in HABARI
0
NMB YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA HOSPITALI YA MICHEWENI PEMBA
0
SHARES
35
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

 

 

RelatedPosts

DIAMOND KANILIPA MILIONI 17 VIDEO YA ZUWENA

DIAMOND KANILIPA MILIONI 17 VIDEO YA ZUWENA

Feb 5, 2023

VIJANA ACHENI KU-BET FANYENI KAZI – CHONGOLO

Feb 5, 2023

RAIS WA ZAMANI WA PAKISTAN AFARIKI DUNIA

Feb 5, 2023
Load More
Rais wa Zanzibar na mwenyekikti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi (wapili kulia) akipokea moja ya viti venye magurudumu kutoka kwa Meneja wa Biashara wa Zanzibar wa Benki ya NMB, Naima Shaame (watatu kushoto) wakati akizindua hospitali ya wilaya ya Micheweni, Kaskazini Pemba. Benki ya NMB imetoa msaada wa vifaa venye thamani ya zaidi ya shilingi milioni tisa katika uzinduzi wa Hospitali hiyo.

 

Benki ya NMB imetoa msaada wa vifaa vya tiba mbalimbali kwa Hospitali ya Wilaya ya Micheweni Pemba ikiwa ni utekelezaji wa azma yake ya kusaidia utoaji wa huduma bora za afya.

Mchango wa benki hiyo unaenda sambamba na maadhimisho ya miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar mwaka huu.

Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na mashuka 200, mapazia ya wodini wodini 10, viti vya magurudumu 5 kwaajili ya kusaidia wagonjwa na mashine tatu za kupimia presha.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika katika Hospitali ya Wilaya ya Micheweni Pemba, Meneja wa NMB Tawi la Zanzibar, Naima Said Shaame alisema mchango wa benki hiyo unatokana na dhamira yake ya kusaidia ujenzi wa Taifa lenye afya bora.

Aidha, aliongezea kuwa benki yake inatoa kipaumbele kwa sekta ya afya na kusistitza kuwa sekta hiyo ni moja ya nguzo kuu za Mpango wa Uwajibikaji kwa Jamii na inawajibika kwa asilimia moja ya faida baada ya kodi (PAT) kugharamia mipango mbalimbali ya kijamii katika maeneo yake ya kipaumbele ikiwemo afya, elimu na dharura.

ADVERTISEMENT

Na mpaka sasa, imechangia kwa kiasi kikubwa katika hospitali mbalimbali nchini na kuongeza kuwa michango ya benki hiyo inaleta mabadiliko makubwa katika kuinua viwango vya utoaji wa huduma za afya nchini kote.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk Hussein Mwinyi akiwa ni mgeni rasmi wa uzinduzi huo, alipokea vitu hivyo kwa niaba ya Hospitali ya Wilaya na kuishukuru benki hiyo kwa ukarimu wake na kuongeza kuwa uzinduzi wa Hospitali ya Wilaya ya Micheweni ni njia bora ya kuadhimisha miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar mwaka huu.

Lakini pia, aliwataka watoa huduma wa Hospitali hiyo ya Wilaya kutoa huduma bora kwa wateja kwani ni sehemu muhimu katika utoaji wa huduma za afya huku Waziri wa Afya Zanzibar Mhe, Nassor Ahmed Mazrui alisisitiza dhamira ya Wizara yake ya kutunza miundombinu katika Hospitali ya Wilaya ya Micheweni ili kutoa huduma bora za afya kwa Wazanzibari wote bila ya ubaguzi.

MWISHO

ADVERTISEMENT

Related

ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

DIAMOND KANILIPA MILIONI 17 VIDEO YA ZUWENA
HABARI

DIAMOND KANILIPA MILIONI 17 VIDEO YA ZUWENA

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023
VIJANA ACHENI KU-BET FANYENI KAZI – CHONGOLO
HABARI

VIJANA ACHENI KU-BET FANYENI KAZI – CHONGOLO

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023
RAIS WA ZAMANI WA PAKISTAN AFARIKI DUNIA
HABARI

RAIS WA ZAMANI WA PAKISTAN AFARIKI DUNIA

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023
IDADI YA WALIOFARIKI AJALI YA TANGA YAONGEZEKA HADI 20
HABARI

IDADI YA WALIOFARIKI AJALI YA TANGA YAONGEZEKA HADI 20

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023
MANGE KIMAMBI AMCHANA  HAJI MANARA ‘WE NI MTU MZIMA’
HABARI

MANGE KIMAMBI AMCHANA HAJI MANARA ‘WE NI MTU MZIMA’

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023
NAJUA UCHUNGU WA MTOTO SIWEZI – WOLPER
HABARI

NAJUA UCHUNGU WA MTOTO SIWEZI – WOLPER

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
January 2023
M T W T F S S
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031  
« Dec   Feb »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In