Rapper anayetikisa kitaa na hit song ifahamikayo kama “SIMU” @younglunya (MBUZI) Amfunguka kwamba anatoza kiasi cha Dola za Kimarekani 2500 ambayo ni zaidi ya Milioni 5 za Kitanzaia kwa ajili ya Vesi moja pale ukitaka kufanya naye kazi, Amesema hayo kupitia Xxl Ya Clouds FM
–
–
“Kwenye kulipisha kolabo nangalia vitu vingi kwasababu hii ni kazi mwisho wa siku huwezi kusema silipishi kwa Vesi lakini pia siwezi kusema namlipisha kila mtu, kuna watu wengine kwa mfano wanakuja wana kipaji na uwezo wa kufanya muziki mzuri na amekuja na wimbo wake mzuri na hana uwezo wa kukupa wewe kitu chochote hiyo ni kazi ambayo naifanya bure kabisa Ila nakuwa na baadhi ya haki kwenye digital platforms zake, lakini kwa asanii ambaye anajiweza kabisa amekuja tufanye kazi kiwango cha juu ni Dola za Kimarekani 2500 kwa Vesi, kwa Bar 16”