ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Monday, February 6, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

Pesapal Yaja na suluhisho la kisasa kusimamia uendeshaji wa vituo vya mafuta

I am Krantz by I am Krantz
Jan 25, 2023
in HABARI
0
Pesapal Yaja na suluhisho la kisasa kusimamia uendeshaji wa vituo vya mafuta
0
SHARES
21
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

RelatedPosts

DIAMOND KANILIPA MILIONI 17 VIDEO YA ZUWENA

DIAMOND KANILIPA MILIONI 17 VIDEO YA ZUWENA

Feb 5, 2023

VIJANA ACHENI KU-BET FANYENI KAZI – CHONGOLO

Feb 5, 2023

RAIS WA ZAMANI WA PAKISTAN AFARIKI DUNIA

Feb 5, 2023
Load More
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT
Mfanyakazi was Lake oil akimgudumia mteja.kampuni ya Pesapal imezindua suluhisho inayowawezesha wamiliki wa vituo vya mafuta kuweza kufuatilia na kusimamia mauzo bila kuwepo vituoni.
Mfanyakazi was Lake oil akimgudumia mteja.kampuni ya Pesapal imezindua suluhisho inayowawezesha wamiliki wa vituo vya mafuta kuweza kufuatilia na kusimamia mauzo bila kuwepo vituoni.

 

 

Na Mwandishi Wetu

Kampuni ya huduma za malipo ya Pesapal imeanzisha huduma mpya ya kusaidia kusimamia uendeshaji wa vituo vya mafuta na mauzo ya nishati nyingine unaotumia teknolojia za kisasa na kufanya kazi kiotomatiki.

Viongozi wa kampuni hiyo wamebainisha kuwa lengo kuu la suluhisho hiyo ni hasa kuwasaidia wamiliki wa vituo hivyo kupunguza gharama za uendeshaji na kuongeza ufanisi katika biashara ya reja reja ya mafuta.

Kupitia teknolojia hii, Pesapal imejipanga kuhakikisha hadi mwisho wa mwaka huu vituo 100 vya mafuta kwenye masoko ya Tanzania, Kenya na Uganda vitakuwa vinatumia mfumo huu mpya.

Kitaalamu na kibiashara suluhisho hili linajulikana kama  Pesapal Forecourt Management Solution (PFMS).

Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam, kampuni hiyo imesema PFMS ndilo jibu la takwa la wenye vituo vya mafuta la kuwa na muunganiko wa vifaa vya mauzo usiokuwa na hitilafu yoyote…

Pia PFMS ina uwezo mkubwa wa kusimamia na kufuatilia kwa karibu sana jinsi uuzaji mafuta unavyofanyika. Uwezo huu ndio unaipa suluhisho hii sifa ya kupunguza gharama za uendeshaji lakini pia kusaidia kuondokana na ulaghai huku ikiboresha namna wateja wanavyohudumiwa kwa mawanda mapana ya koungeza mauzo.

“Suluhisho ya PFMS inawezesha wamiliki wa vituo vya mafuta kuweza kufuatilia na kusimamia bila kuwepo vituoni mauzo ya gesi na mashine za kujazia mafuta, mfumo wa vipimo vya matenki, bodi za bei na jinsi malipo yanavyofanyika,” Pesapal ilibainisha katika taarifa yake.

Mwezi Februari mwaka jana Pesapal ilipata kibali cha kutoa suluhisho jumuishi za malipo kwa vituo vya mafuta kutoka kwa jukwaa la kimataifa la viwango la IFSF. Taasisi hii ni jumuiya ambayo imejikita zaidi kufanikisha kuwepo teknolojia za viwango vya kimataifa kwa ajili ya kusaidia kuboresha uendeshaji wa vituo vya mafuta ya magari na nishati nyingine.

Akizungumza hivi karibuni kwenye utambulisho wa PFMS katika masoko ya ukanda huu, Afisa Mtendaji Mkuu wa Pesapal Limited, Bw Agosta Liko, alibainisha umuhimu wa kuufanya mchakato mzima wa usimamizi wa mafuta kuwa wa kiotomatiki.

Uwekezaji huu, kiongozi huyo alifafanua, hutengeneza mazingira mathubuti katika sekta ya reja reja ya mafuta na kuimarisha eneo mtambuka la biashara hiyo kwa hasa kupunguza gharama za uendeshaji na kuimarisha huduma kwa wateja.

Bw Liko alisema matumizi ya suluhisho ya PFMS ili kusaidia zaidi kurahisisha malipo kwenye vituo vya kuuzia mafuta yatafanyika kwa ushirikiano wa kimkakati kati ya Pesapal na wamiliki wa vituo husika.

“Katika nyanja inayobadilika kwa kasi kama hii ya usimamizi wa kuuza mafuta reja reja, zinahitajika suluhisho ambazo ni za kisasa na zinazoanzisha mienendo mipya ya kufanya mambo,” alisisitiza.

Kwa mujibu wa Meneja wa Pesapal Tanzania, Bi Bupe Mwakalundwa, pamoja na suluhisho yao kuwa bunifu zaidi pia inazingatia sana kuwapa wenye biashara ya vituo vya mafuta uwezo wa kuboresha huduma kwa wateja na kuwahudumia watu wengi kwa ufanisi mkubwa.

“Hii suluhisho uwapa wateja fursa ya kufanya manunuzi yao kwa mkupuo wa muamala mmoja, huku wasimamiaji wa vituo vya mafuta wakiwezeshwa kuidhinisha miamala haraka na kwa usalama,” Bi Mwakalundwa alinukuliwa katika taarifa ya Pesapal kwa vyombo vya habari.

Pesapal Limited ni kampuni kinara wa huduma za malipo inayohusika na zana za kuchakata malipo zikiwemo zile za kidijitali na kimtandao hususani kwa ajili ya mashirika ya kibiashara na taasisi nyingine zenye mwelekeo huo.

Pesapal ilianzishwa mwaka 2009 na kwa sasa hivi inafanya biashara katika nchini sita za Kiafrika ambazo ni pamoja na  Zambia, Zimbabwe and Malawi.

Kwa hapa nchini, imekuwepo tangu Julai mwaka jana baada ya kupata idhini ya Benki Kuu kutoa huduma za malipo yasiyohusisha pesa taslimu chini ya Sheria ya Mifumo ya Malipo ya Taifa ya Mwaka 2015.

MWISHO….

Related

ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

DIAMOND KANILIPA MILIONI 17 VIDEO YA ZUWENA
HABARI

DIAMOND KANILIPA MILIONI 17 VIDEO YA ZUWENA

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023
VIJANA ACHENI KU-BET FANYENI KAZI – CHONGOLO
HABARI

VIJANA ACHENI KU-BET FANYENI KAZI – CHONGOLO

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023
RAIS WA ZAMANI WA PAKISTAN AFARIKI DUNIA
HABARI

RAIS WA ZAMANI WA PAKISTAN AFARIKI DUNIA

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023
IDADI YA WALIOFARIKI AJALI YA TANGA YAONGEZEKA HADI 20
HABARI

IDADI YA WALIOFARIKI AJALI YA TANGA YAONGEZEKA HADI 20

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023
MANGE KIMAMBI AMCHANA  HAJI MANARA ‘WE NI MTU MZIMA’
HABARI

MANGE KIMAMBI AMCHANA HAJI MANARA ‘WE NI MTU MZIMA’

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023
NAJUA UCHUNGU WA MTOTO SIWEZI – WOLPER
HABARI

NAJUA UCHUNGU WA MTOTO SIWEZI – WOLPER

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
January 2023
M T W T F S S
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031  
« Dec   Feb »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In