Aliyekuwa mgombea Urais nchini Kenya kupitia muungano wa Azimio Raila Odinga ametangaza kutotambua matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2022 na matokeo yake.
–
Odinga na viongozi wengine wa Upinzani wameanza maandamano na mikutano ya hadhara nchini Kenya wakidai kuwa ni kwa ajili ya kuonesha ushahidi jinsi uchaguzi huo ulivyovurugwa.
ADVERTISEMENT
–
“Sisi, kama Azimio, tunakataa matokeo ya uchaguzi wa 2022. Hatuwezi na hatutatambuu utawala wa Kenya Kwanza na hatumtambui Bw. William Ruto kama Rais wa Kenya na vile vile hatuwatambui maafisa wowote walio ofisini naye” amesema Odinga