Uongozi wa Klabu ya Simba leo majira ya mchana Januari 26,2023 umemtangaza rasmi Imani Kajula kuwa mwajiliwa katika klabu hio akienda kukaimu nafasi ya Afisa Mtendaji mkuu (CEO) kwa mkataba wa miezi sita.
Kajula anaziba nafasi iliyoachwa na Barbara Gonzalez ambaye alitangaza kujiuzulu katika nafasi hio Disemba 10 Mwaka jana.
Kabla ya kujiunga na nafasi hio katika klabu ya Simba, aliwahi kuwa Mtendaji mkuu wa Kampuni ya Masoko na Mawasiliano ya EAG Group tangu mwaka 2013.Zaidi ya hapo inaelezwa kuwa Kajula ni mzoefu katika masuala ya uongozi katika mpira kwani aliwahi shiriki kwenye kamati ya maandalizi ya Michuano ya Afrika kwa Vijana chini ya umri wa miaka 17 iliyofanyika nchini mwaka 2019.