ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Monday, February 6, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

TATHMINI VYANZO VYA MAPATO KUFANYIKA HALMASHAURI ZA NCHINI KUJITEGEMEA

Ruvuma

ALFRED MTEWELE by ALFRED MTEWELE
Jan 17, 2023
in HABARI
0
TATHMINI VYANZO VYA MAPATO KUFANYIKA HALMASHAURI ZA NCHINI KUJITEGEMEA
0
SHARES
17
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

RelatedPosts

Dkt. Jafo: “Huenda zaidi ya Sh. Trilioni 1 Zikapatikana kwa Mwaka Kutokana na Biashara ya Kaboni”

Dkt. Jafo: “Huenda zaidi ya Sh. Trilioni 1 Zikapatikana kwa Mwaka Kutokana na Biashara ya Kaboni”

Feb 3, 2023

Bilioni 213 za Miradi ya DMDP Zaistawisha Temeke

Feb 2, 2023

DKT. DUGANGE-95% YA ZABUNI ZA TARURA KAZI INAENDELEA

Jan 24, 2023
Load More
May be an image of 6 people, people standing and people sitting
MKURUGENZI wa Sera na Mipango Ofisi ya Rais TAMISEMI John Mihayo Cheyo amesema ofisi yake inafanya zoezi la tathimini ya ukusanyaji wa mapato katika Halmashuri zote 184 Tanzania Bara.
Amesema zoezi hilo limeanza Januari 9 mwaka huu na linafanyika kwenye Halmashauri na mikoa yote mchini na kwamba linajumuisha wataalam kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI,Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA,Wizara ya Fedha,Ofisi ya Mkoa husika na Halmashauri zake.
Akizungumza katika mahojiano maalum Mkoani Ruvuma,Mkurugenzi huyo wa Sera na Mipango amesema kwa ujumla wakurugenzi wa Halmashauri nchini kote wamefurahia zoezi la tathimini ya ukusanyaji wa mapato na wameshauri liwe zoezi endelevu.
“Zoezi hili la tathimini ya ukusanyaji mapato ambalo linafanyika nchi nzima linaweza kutuongezea mapato mengi kwenye Halmashauri na hatimaye kuzifanya Halmashauri zetu kuanza kujitegemea’’, alisisitiza Cheyo.
Hata hivyo amesema kukamilika kwa zoezi hilo kutawezesha kufanya makisio ya mapato kwa uhalisia katika Halmashauri kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024.
Mkurugenzi huyo anawapongeza viongozi wote wa TAMISEMI,Kamishina Mkuu wa TRA na makatibu tawala wa mikoa yote nchini kwa kusimamia kikamilifu zoezi la tathimini ya ukusanyaji mapato.
Kwa upande wake Mchumi Ofisi ya Rais TAMISEMI Flugence Matemele ambaye alikuwa kiongozi wa Timu ya Tathimini ya kusanyaji mapato ya ndani kwenye Halmashauri za mkoa wa Ruvuma,amesema zoezi limekwenda vizuri na wakurugenzi wa Halmashauri wametoa ushirikiano wa kutosha.
Amesema katika tathimini hiyo wamefanikiwa kuchambua chanzo cha mapato kimoja kimoja kwa kila Halmashauri kuanzia vyanzo vikubwa wanavyojitegemea ambavyo vimebainika vinachangia mapato kuanzia asilimia 22 hadi 58.
Matemele amesema wakati wanafanya uchambuzi huo wamebaini kuna uwekezekano mkubwa wa vyanzo hivyo vya mapato kukusanya mapato mengi zaidi kama vitasimamiwa kwa nguvu zaidi.
“Wakurugenzi wa Halmashauri na watalaam wao wamethibitisha bado walikuwa wanafanya makisio ya bajeti ya kukusanya vyanzo vya mapato kwa kutumia uzoefu tu,lakini katika tathimini hii tumewasisitiza kutumia takwimu’’,alisema Mchumi wa TAMISEMI.
Hata hivyo ameitaja changamoto ambayo imeonekana kwenye tathimini hiyo kuwa ni wataalam kufanya makisio bila kuzingatia takwimu ambapo wataalam hao wameahidi kuanzia sasa watafanya makisio yenye uhalisia.
Amesema zoezi hilo la tathimini ya kusanyaji mapato limeiungaisha TAMISEMI na Taasisi muhimu kama TRA ili kushirikiana na Halmashauri katika uboreshaji ukusanyaji mapato ya ndani katika Halmashauri zote nchini.
Naye Mchumi Mwandamizi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Henry Kaiwanga amesema katika tathimini ya ukusanyaji mapato walioufanya katika Halmashauri za Mkoa wa Ruvuma wamebaini kuwa vyanzo vikuu vya mapato ni mazao ya kilimo,misitu na madini ambapo wamebaini makusanyo yanayokusanywa ni kiwango kidogo sana kutokana na makadirio ya chini wanayoweka.
Hata hivyo amesema wamebaini changamoto ya tofauti ya takwimu kwenye ukusanyaji mapato kati ya TRA na Halmashauri husika ambapo imebainika Halmashauri ina takwimu zake na TRA ina takwimu zake hali inayochangia makusanyo hafifu.
Amesema kutokana na tathmini hiyo wameshauri maafisa mapato wa TRA na maafisa wa Halmashauri kufanya kazi kwa Pamoja ili Taasisi zote mbili zikusanye mapato zaidi.
Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Jumanne Mwankoo ameipongeza Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kufanya zoezi hilo ambalo limekuwa na umuhimu mkubwa katika kuboresha mapato ya ndani katika Halmashauri zote nchini.
Amesema zoezi hilo limeongeza uelewa kuhusu makisio ya mapato ya ndani kwenye Halmashauri kwa sababu wataalam walikuwa wanafanya makisio kwa mazoea.
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

Related

Tags: OFISI YA RAIS TAMISEMI
ADVERTISEMENT
ALFRED MTEWELE

ALFRED MTEWELE

Related Posts

DIAMOND KANILIPA MILIONI 17 VIDEO YA ZUWENA
HABARI

DIAMOND KANILIPA MILIONI 17 VIDEO YA ZUWENA

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023
VIJANA ACHENI KU-BET FANYENI KAZI – CHONGOLO
HABARI

VIJANA ACHENI KU-BET FANYENI KAZI – CHONGOLO

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023
RAIS WA ZAMANI WA PAKISTAN AFARIKI DUNIA
HABARI

RAIS WA ZAMANI WA PAKISTAN AFARIKI DUNIA

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023
IDADI YA WALIOFARIKI AJALI YA TANGA YAONGEZEKA HADI 20
HABARI

IDADI YA WALIOFARIKI AJALI YA TANGA YAONGEZEKA HADI 20

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023
MANGE KIMAMBI AMCHANA  HAJI MANARA ‘WE NI MTU MZIMA’
HABARI

MANGE KIMAMBI AMCHANA HAJI MANARA ‘WE NI MTU MZIMA’

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023
NAJUA UCHUNGU WA MTOTO SIWEZI – WOLPER
HABARI

NAJUA UCHUNGU WA MTOTO SIWEZI – WOLPER

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
January 2023
M T W T F S S
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031  
« Dec   Feb »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In