Mchezaji Cesar Manzoki amesema Viongozi wa Simba walifanya kila kitu kinachowezekana ili aje Simba lakini Watu wenye roho mbaya hawakutaka “Najua kuna Watu wengi walikuwa wanawaza Mimi ninaweza nikavaa rangi ya kinyokanyoka lakini Simba anabakia Simba”
–
Akiongea kwenye Mkutano Mkuu wa Simba leo Manzoki amesema “Mimi ni Mwana Simba na kama kuna Klabu Afrika ambayo ninaweza nikacheza ni Simba tu hakuna kingine”
–
Cesar Manzoki ni Mchezaji wa Afrika ya Kati mwenye asili ya Congo DR ambaye alikuwa anachezea Vipers SC ya Uganda na baadaye Simba kuhusishwa kumsajili na kwa 90% kila kitu kilienda sawa.
–
Dakika za mwisho wakati Simba wako katika mazungumzo na Vipers SC, wakashindwana wakati huo Mchezaji na Simba wakiwa wamemalizana, kwakuwa alikuwa na mkataba na Vipers basi ikaamua kumuuza kwenda club ya Dalian Pro ya Ligi Kuu nchini China.
–
Credit – Millard Ayo