Jeshi la polisi mkoani Kagera limewaua watu wawili katika barabara ya Kumunazi – Rulenge wilayani Ngara na kuwakuta wakiwa na bunduki moja AK-47, kibeba risasi (magazini) iliyokuwa na risasi 25 pamoja na mabomu mawilii ya kurusha kwa mkono.
–
Kamanda wa polisi mkoani Kagera, William Mwampaghale amesema walipata taarifa ya kuwepo kwa watu watatu waliokuwa wakisafiri kwa kutumia pikipiki wakiwa na silaha.
–
“Tuliweka mtego katika eneo la Kumunazi na watu hao watatu wakiwa kwenye pikipiki walitokea na walisimamishwa na laikini walikaidi na kugeuza pikipiki kurejea walipotokea”.
–
“Waliitwa mara kadhaa na maafisa wa polisi lakini walikaidi na kuwalazimisha polisi kufyatua risasi ambazo ziliwaumiza watu wawili na mmoja aliyekuwa akiendesha pikipiki alifanikiwa kutoroka”.
–
Ameongeza kamanda Mwampaghale Watu hao wawili waliojeruhiwa na risasi walikutwa wakiwa na bunduki moja AK-47 na kibeba risasi chenye risasi 25 sambamba na mabomu mawili ya kurusha kwa mkono.
–
Miili ya marehemu hao wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 25-30 imehifadhiwa katika hospital ya Nyamihaga wilayani Ngara kwa ajili ya utambuzi na uchunguzi zaidi.