Waziri mwenye dhamana ya Afya nchini Tanzania Mh. Ummy Mwalimu ameendeleza jitihada za kusisitiza wananchi kuweza kujiunga na bima kupitia nukuu zake ambazo zinaonesha kwa jinsi gani bima inagusa moja kwa moja katika kujilinda na athari zihusuanazo na afya ambazo zinaweza kujitokeza katika siku za usoni.
“Sisi kama Serikali tunatambua mchango wa Wahariri kusimamia utoaji wa habari na kuelimisha wananchi, lakini pia kukosoa pale inapoonekana inafaa “ Mhe. @ummymwalim, Waziri wa Afya.
“Nawahimiza Watanzania kuanza kudunduliza ili kujiwekea uhakika wa matibabu kabla ya kuugua kwa kujiunga na mifuko ya bima ya afya. Hautalazimishwa kujiunga na mfuko wa umma lakini unaweza kuchagua mifuko ya bima za binafsi ila kutakua na kitita cha mafao ya msingi”@ummymwalimu
“Sheria hii tunayotunga siyo msaafu wala biblia,endapo huko mbeleni tutaona changamoto tutafanya marekebisho ndiyo maana baadhi ya mambo tunayaweka kwenye kanuni ili iwe rahisi kupokea maoni kutoka kwa wadau na kuyafanyia marekebisho pale ambapo tumeona hapako vizuri”
“Katika kutekeleza Bima ya Afya kwa Wote tunaenda hatua kwa hatua, tunaamini kwamba wachache watakaojiunga wakaona manufaa na faida ya bima ya afya watakua chachu ya kuwashawishi wengine wajiunge lakini pia Serikali itaendelea kuimarisha huduma za afya ili kiwe kishawishi” Ummy
“Tumesema Bima ya Afya kwa wote ni lazima ila hakuna kosa la kisheria hapo, hakuna mtanzania atakamatwa, kuwekwa ndani au kufungwa kwa kukosa Bima ya Afya. Ila tunakwambia ukitaka kupata leseni ya biashara basi uwe na Bima ya Afya.” Waziri @ummymwalimu
“Bima ya afya ni kwa ajili ya kumsaidia Mtanzania hususan masikini, kwa sasa Mtanzania masikini akiumwa atauza mali zake alizonazo ili apate matibabu, wapo wanaouza pikipiki, viwanja ili tu kumudu gharama za matibabu” Mhe.@ummymwalimu, Waziri wa Afya
“Tumekwenda Rwanda, Ghana hizi ni nchi za Afrika. Mfano Rwanda polisi anakusimamisha barabarani anakagua Bima ya Afya ipo wapi, sisi tunauliza bima ya gari tunakagua matairi ila wenzetu wanakagua bima ya afya kwa sababu ni lazima.” Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.
“Tuna kesi zenye ushahidi watanzania wanauza nyumba zao ili kugharamia matibabu ya mgonjwa, Bima ya Afya ni moja ya sehemu ya kumkomboa mwananchi maskini kwa sababu atapata huduma za matibabu bila ya kikwazo cha fedha.” Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu
ADVERTISEMENT